LIVE STREAM ADS

Header Ads

NUSRA POLISI WATUMIE MABOMU YA MACHOZI KUWATAWANYA WAFUASI WA CHADEMA JIJINI MWANZA.


Askari wa kutuliza ghasia Jijini Mwanza, wakijaribu kuwatuliza wafuasi wa Chadema waliokuwa wametanda katika barabara inayotoka Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza hii leo, wakifuatilia hatma ya kesi ya kupinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Octoba 25,2015 Jimbo la Nyamagana.

 Katika kesi hiyo aliekuwa mgombea ubunge jimbo la Nyamagana (Chadema) Ezekiel Wenje anapinga ushindi wa Mbunge wa jimbo hilo Stanslaus Mabula (CCM).

Mahakama imeanza kusikiliza ushahidi wa upande wa mlalamikaji hii leo na imefanikiwa kusikiliza mashahidi wawili kati ya 14 wa upande wa huo na kesi imeahirishwa hadi Machi 16,2016 jumatano wiki hii.
Na:Binagi Blog
Zaidi BONYEZA HAPA

No comments:

Powered by Blogger.