MNYUKANO MKALI WAENDELEA KESI YA WENJE JIJINI MWANZA.
Mawakili wakiteta jambo kabla kesi haijaanza kusikilizwa.
Na:George Binagi-GB Pazzo
Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza leo imeahirisha
kusikiliza Ushahidi katika kesi ya Kupinga Matokeo ya Uchaguzi Mkuu Jimbo la
Nyamagana Mkoani.
Jaji wa Mahakama hiyo, Kakusulo Sambo ameahirisha
kesi hiyo ambayo iliyofunguliwa na aliekuwa mgombea wa Chadema Ezekiel Wenje anaepinga ushindi wa Stanslaus Mabula (CCM) kwa madai kwamba uchaguzi haukuwa wa huru na haki, hadi
kesho majira ya saa tatu asubuhi ili kutoa fursa kwa mawakili wa wajibu maombi kujiandaa
kwa ajili ya kujibu hoja za mawakili wa mleta maombi.
Mawakili wa Mjibu maombi wakiongozwa
na Wakili Constantin Mtalemwa waliiomba Mahakama kuahirisha kesi hiyo hadi
April Mosi, ili kujiandaa kujibu hoja za mawakili wa mleta maombi wanaoongozwa
na Wakili Deya Outa ambapo hata hivyo ombi hilo lilikataliwa na Mahakama na
hivyo kuamuru hoja hizo kujibiwa kesho machi 31.
Awali Mawakili wa Mleta maombi
waliiomba Mahakama hiyo kutoa idhini ya kusikiliza ushahidi unaotokana na vielelezo
vya fomu za uchaguzi nambari 21 B, baada ya moja ya fomu hizo ambazo jumla yake
ni 646 kuwekewa pingamizi kutokana na kutowasilishwa mahakamani hapo na
wahusika kwa muda mwafaka.
Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza inaombwa
kutenda haki katika kesi hiyo hususani kuzingatia muda wa kutoa maamuzi yake. Hii leo hakukuwa na wafuasi wengi wa vyama vya siasa kama ilivyoonekana awali katika kesi hii ambapo upande wa usalama hali ya ulinzi imeendelea kuimarishwa katika viunga vya Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza.
Wakili Upande wa Mleta Maombi, Deya Ouma
Mabula na Wenje, wote hawakuwa mahakamani hapo hii leo.
No comments: