LIVE STREAM ADS

Header Ads

RC SHINYANGA ACHARUKA KUHUSU WATUMISHI HEWA.

Na:Shaban Njia
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anna Kilango Malecela ametoa muda wa siku sita kwa Wakurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kahama, kuhakikisha wanawasilisha majina ya Watumishi hewa katika Ofisi yake.

Mkuu huyo wa Mkoa aliyasema hayo wakati akizungumza na watumishi wa Halmashuri zote tatu za Wilaya ya Kahama, muda mfupi baada ya kumaliza ziara yake ya siku moja ya kukagua shughuli za maendeleo ikiwa ni pamoja na kuwapa pole wahanga wa  mvua ya mawe wa Mwakata.

Kilango alisema kuwa kuna rundo la watumishi hewa wanaofanya kazi katika Halmashauri hizo, hivyo ni wajibu kwa wakurugenzi kwa sasa kuhakikisha kuwa majina yao yanawasilishwa katika ofisi yake pamoja na maelezo ya waliajiriwa lini, wanalipwaje, na kiasi gani wanalipwa.
Muda wa agizo hilo unafikia tamati tarehe 30 mwezi huu.

No comments:

Powered by Blogger.