LIVE STREAM ADS

Header Ads

SHULE YA MSINGI NYAWILIMIMILWA MKOANI GEITA YAELEMEWA.

SHULE Msingi Nyawilimilwa iliyopo katika halmashauri ya wilaya ya Geita ndiyo shule pekee iliyoandikisha idadi kubwa ya wanafunzi wa darasa la kwanza Mkoani Geita, kutokana na mwamko wa wazazi kusomesha watoto wao, baada ya serikali kutangaza elimu bure.


"Wanafunzi wa darasa la kwanza ni 2,052, darasa la awali ni wananfunzi 314, darasa la MEMKWA ni wanafunzi 210. Darasa la kwanza hadi la Saba kuna jumla ya wanafunzi 4,821. Shule hii ina jumla ya madarasa 11 tu, na kuna uhitaji wa madarasa 82, inamatundu ya vyoo 18 mahitaji ni 76, nyumba za walimu zipo tisa huku mahitaji yakiwa ni 82". Anasema Mkuu wa shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 1975, Mwalimu Mawazo Mayunga.

No comments:

Powered by Blogger.