LIVE STREAM ADS

Header Ads

SIKU YA WANAWAKE DUNIANI, KUDAI HAKI AMBAZO ZIMEKUWA ZIKIDAIWA KWA MIAKA 100 NI KUIGIZA.

Na:Nyakorema Rioba
Tunaposherehekea Siku ya Mwanamke Duniani, ambayo ilianza kusherehekewa tangu mwaka 1907, kama tutaendelea kudai haki ambazo zimedaiwa kwa zaidi ya miaka 100, tutakuwa tunaigiza kila march 8.

Haki gani? Kama naweza soma Engineering na nikafaulu zaidi ya wavulana, nadai haki ipi? kama naweza beba ujauzito, nikajufungua, nikalea, nikawa career woman, mke na mama wa familia, nadai haki gani?

Haki tunazo ni wakati wa KUZITUMIA na zilete maendeleo. Ni wakati wa kumkumbusha/ kumuelimisha mama wa kijijini kuwa kumkeketa mwanae ni kuudhalilisha utu wake, ni wakati wa kumkumbusha yule mke kwamba, kupigwa na mume sio kawaida, ni jambo BAYA na kuudhalilisha utu wake. Ni wakati wa kumkumbusha na kumpa elimu yule mama, yule mtoto na yule baba. SI WAKATI WA KUDAI HAKI.

Tuwaheshimu waume zetu hata kama tutakuwa na digrii tano, nao watupende as their equal human being, we are human being (men and women).

Elimu BORA kwa mtoto wa kike na wa kiume ndio zitakomboa taifa. Tuwambie mabinti zetu na vijana wetu kwamba, SISI NI BINADAMU, Tunawezafanya lolote wote kwa pamoja, tofauti yetu ni maumbule tu.

WOMEN, lets step out and be WOMEN we were meant to be. Lets discuss ideas and not people, lets admire the giant mind and not small mind, lets have dreams and not fights, lets pray for each other and not gossip. Ni sisi wenyewe TUNAJISHUSHIA HADHI. Heroes are the men who support their wives and bring the best out of them. I SALUTE YOU.

No comments:

Powered by Blogger.