TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI: TAMKO LA WARATIBU WA CHASO MIKOA.
CHAMA CHA
DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA).
CHADEMA STUDENTS’ ORGANIZATION (CHASO).
TAMKO LA WARATIBU WA CHASO MIKOA
Ndugu zangu
waandishi, habarini, tumewaiteni hapa ili muweze kutusaidia kuupeleka ujumbe
huu kwa watanzania na wahusika.
Kwanza
tunaunga mkono tamko la kamati kuu ya chama lililotolewa jana na mwenyekiti wa chama
kwa vyombo vya habari.
1. UCHAGUZI
WA MEYA WA JIJI LA DAR ES SALAAM
Kwanza tunasikitika takribani siku zaidi
ya 100 zimepita tangu kufanyika uchaguzi mkuu 2015, wa urais, wabunge na madiwani
lakini cha kushangaza jiji la Dar es Salaam mpaka leo halina Meya ambapo kisheria
ilipaswa awe amepatikana ili akawahudumie wananchi lakini tunashuhudia matumizi
makubwa ya vyombo vya dola dhidi ya madiwani na wabunge wa UKAWA.
Tumeshuhudia RAS wa mkoa wa Dar es
Salaam akitumia amri bandia ya mahakama kwa kukwamisha uchaguzi usifanyike,
lakini hajachukuliwa hatua za kisheria mpaka sasa. Tunavitaka vyombo vinavyohusika
vimchukulie hatua mara moja, vinginevyo tutaendekeza upotoshwaji na uvunjwaji wa
sheria katika nchihii.
Pia tunawataka wenzetu wa CHAMA CHA
MAPINDUZI wakubali kushindwa na waheshimu maamuzi ya wananchi wa Dar es Salaam
waliowachagua kwa wingi madiwani na wabunge wa UKAWA ili waliongoze jiji la Dar
es Salaam kwa miaka mitano ya kikatiba.
Tunahimiza uchaguzi huu ufanyike haraka
ili wananchi wa Dar es Salaam wapate haki ya kutatuliwa kero mbalimbali,
kupitia viongozi waliowachagua. Pia tunalitaka jeshi la polisi liache kuwanyanyasa
na kuwadhalilisha madiwani na wabunge wetu, kama ambavyo wamefanya Kilombero,
Dar es Salaam, Kyerwa na Zanzibar.
2. HALI
YA ELIMU NCHINI
Ndugu zangu waandishi wa habari tumeshuhudia
hivi karibuni, wizara ya elimu kupitia tume ya vyuovikuu nchini (TCU) ikivifutia
usajili baadhi ya vyuovikuu nchini, kama vile matawi ya St. Joseph Songea na Arusha,
na baadhi ya vitivo katika Chuo Kikuu cha Kampala Dar es Salaam.
Hivi ni viashiria vya anguko la elimu nchini,
tunahoji ni kwanini TCU awali ilikubali kuvisajili vyuo hivi na baadae
kuvifuta? Je vyuo hivi vinafutiwa usajili kwa sababu havijakidhi vigezovya kuwa
vyuo vikuu? Kama ni ndiyo,vyuo hivi vimezalisha wataalamu wasiokidhi vigezo katika
kada mbalimbali, hivyo tunavitaka vyombo vinavyohusika kuwachukulia hatua za kisheria
tume ya vyuo vikuu Tanzania (TCU) mara moja kwa kuhusika moja kwa moja katika maporoko
ya elimu Tanzania.
Jambo hili limesababisha usumbufu kwa wanafunzi
katika vyuo hivi, tunaitaka serikali ichukue hatua za haraka kuwasaidia wanafunzi
hawa kupata vyuovingine navile vile iwalipe fidia kwa usumbufu uliojitokeza.
Vile vile tunaiomba serikali kupitia
wizara ya elimu kuangalia upya mfumo wa utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu
ya juu, ni wazi kwamba fedha hizi haziwanufaishi wanafunzi wanaotoka katika mazingira
magumu kuweza kugharamia elimuyao, vile vile serikali ichukue hatua za haraka
kuwasaidia wanafunzi wasio na mikopo vyuoni ili waweze kupata haki yao ya
kupata elimu.
Suala la elimu bure bado ni changamoto,
kwani pesa zilizotolewa kwa awamu ya kwanza hazikuweza kukidhi utoajiwa elimu katika
shule mbalimbali hapa nchini, kwa mfano shule ya msingi Chiseyu iliyopo Mpwapwa
Dodoma yenye wanafunzi zaidi ya 780 ilipewa kiasi cha Tshs 29,000/=, kwa mazingira
hayo ni wazi kwamba sera hii itadumaza hali ya elimu, lengo la watanzania siyo kupata
elimu bure tu, bali iwe bure na bora, ili elimu iwe bora serikali inapaswa
kuchukua hatua malimbali kwa mfano kuimarisha miundombinu ya elimu (mishahara inayokidhi
mahitaji ya mwalimu, vifaa vya kufundishia na kujifunzia vilivyo bora).
Serikali itoe onyo kwa Chama cha
Mapinduzi kuingilia Maamuzi ya vyuoVikuu, kwa mfano hivi karibuni tumeshuhudia
Chama cha Mapinduzi kikishinikiza Chuo kumfukuza Mwanafunzi wa Chuo kikuu cha
Dodoma, Victor A. Byemelwa kupitia kwa mshauri
wa wanafunzi (DEAN OF STUDENTS) kwa barua yenye kumbukumu no Re.UDOM/DOS/36 ya
tarehe 5 february 2016.
Imetolewa leo tarehe 06/03/2016 Makao Makuu
CHADEMA
K.N.Y: WARATIBU WA CHASO MIKOA YOTE
TANZANIA
No comments: