LIVE STREAM ADS

Header Ads

HAKIKA HUU MCHEZO HAUHITAJI HASIRA.

"Mchezo Huu Hauhitaji Hasira". Ni neno lililopata umaarufu mkubwa hivi karibuni baada ya Efm Radio ya Jijini Dar kuwanyakua watangazaji maarufu wa Clouds Fm (Dar) ambao ni Paul James (PJ), Gerald Hando na Abel Onesmo, HUKU Clouds wao wakimchukua Gadna G.Habash kutoka Efm, maana waswahili walisema ukimwaga mboga, mwenzio anamwaga ugali.

Awamu nyingine ya mchezo huu imeendelea tena baada ya Clouds Fm kuwasajili, Mtangazaji Mami pamoja na Dj maarufu wa kike nchini, Dj Sinyoritha, wote kutoka EA Radio & Tv.
Inatosha tu kusema kwamba "Hakika Mchezo Huu Hauhitaji Hasira" hivyo Watangazaji waendelee kuchapa kazi ili awamu yao ikifika, wasajiliwe usajili wa uhakika na si wa kiubabaishaji kama ilivyozoeleka hapo awali.

No comments:

Powered by Blogger.