LIVE STREAM ADS

Header Ads

MAJAMBAZI YAVAMIA DUKA LA FEDHA JIJINI MWANZA NA KUUA.

Judith Ferdinand, Mwanza
Matukio ya ujambazi na unyang' anyi  wa kutumia silaha yameendelea kutikisa mkoa wa Mwanza na kusababisha vifo vya watu na majeruhi kadhaa, ambapo jana usiku majambazi wenye silaha wamemuua kwa risasi mfanyabiashara wa duka la huduma za kifedha (M- Pesa,Tigo- Pesa na Airtel money) Monica John(38), mkazi wa mtaa Wa Ibungilo"A" wilayani Ilemela mkoani hapa.

Ikumbukwe ni takribani mwezi tangu kuripotiwa kwa tukio kama hilo,ambalo lilimuhusisha mfanyabiashara Wa M- Pesa Naomi Lewins(35), mkazi wa mtaa Wa Temeke wilayani Nyamagana ambaye inasadikiwa  alipigwa na silaha ya moto kifuani kwenye titi upande wa kushoto na kupoteza maisha hapohapo.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kwa niaba ya Kamanda wa Polisi Mkoa Wa Mwanza Ahmed Msangi, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi Zarau Mpangule alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa majambazi hao wakiwa na silaha aina ya SMG walivamia duka na kumuua mfanyabiashara huyo kwa kumpiga risasi ya kichwa na kufariki hapo hapo kisha kupora fedha kiasi ambacho hakijajulikana.

Alisema, tukio hilo lilitokea Apili 27 mwaka huu, majira ya saa moja jioni katika eneo la mtaa wa Ibungilo Kata ya Nyamanoro wilayani Ilemela mkoani hapa, ambapo majambazi hao wanaosadikiwa ni watatu wakiwa na silaha ya motorcycles walivamia duka hilo ambalo ni mali ya  Thomas Ogango (44) dereva wa lori  na kumuua mfanyabiashara huyo ambaye ni mke wa mmiliki wa duka hilo, mara baada ya kutokea mabishano kati ya marehemu na watuhumiwa wakitaka wapewe fedha.

Pia aliongeza kuwa majambazi hao walipiga risasi hivyo hewani wakati wakiondoka eneo la tukio na kujeruhi watu watatu, ambao ni Joseph Mwita(31) aliyejeruhiwa bega, Fredric Mtayoba(20) fundi  ujenzi aliyejeruhiwa paja na Living Dominician (31) alijeruhiwa goto mguu wa chini, wote ni wakazi wa Ibungilo.

Aidha alisema, majeruhi hao wamelazwa katika hospitali ya Bugando wakipatiwa matibabu na hali zao zinaendelea vizuri.
Haya hivyo  alisema, jeshi la Polisi wako  katika msako mkali wa kuwatafuta watuhumiwa wa mauaji hayo na kuhakikisha wanakamatwa na hatua za kisheria zinachukuliwa dhidi yao.

Vilevile aliwaomba wananchi, vyombo vya habari,wadau wa ulinzi na usalama kushirikiana na jeshi la polisi kwa kutoa taarifa mapema ili waweze kutokomeza uhalifu mkoani hapa.

No comments:

Powered by Blogger.