LIVE STREAM ADS

Header Ads

MGOGORO WA DALADALA NA BAJAJI MKOANI KIGOMA WATATULIWA.

Na Rhoda Ezekiel, Kigoma
Halmashauri ya Kigoma Ujiji katika kuhakikisha inatatua mgogoro baina ya madereva wa bajaji pamoja na daladala, imeamua kutengeneza  vituo vya maegesho ya bajaji.

Akizungumza na Umoja wa madereva  na wamiliki wa Bajaji na Bodaboda (CHAWABOBAKI) Mkuu wa Wilaya ya kigoma, Savery Mwangasame, wakati akikabidhi vituo 16  ambavyo vimekamilika kati ya 50 aliwaomba madereva hao kutumia vituo hivyo kupakia abiria kwa kufuata taratibu.

“Niwaombe madereva bajaji na bodaboda, mpaki katika vituo mlivyo jengewa na Manispaa, ili muweze kuwapa fursa na madereva wa daladala nao kufanya biashara katika maeneo yao”, alisema Mwangasame.

Hata hivyo Mwenyekiti wa  CHAWABOBAKI, Dograsi Kabogo, alisema hawawezi kupokea vituo vichache ambavyo vipo barabara kuu tu kwa sababu  madereva hao ni wengi hivyo watapokea vituo hivyo endapo vitakamilika vyote.

Akitoa taarifa ya mradi huo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa, kaimu mhandisi  wa manispaa ya Kigoma, Wilfred Shimba, alisema mradi huo utaghalimu shilingi milion 29 hadi kukamilisha ujenzi wa vituo 50 ambapo  awamu ya kwanza vimejengwa vituo 16 tu.

Vituo vilivyo kamilika ni Ujiji Heath Centre ,     ACT Ujiji, Anna, Darajani, mnarani, Maweni, Mwangasokoni, Mwanga kwa mchaga, OTTU Mwanga, Website, Kakorwa Road, Msikiti wa Kigoma, Msikiti wa Kigoma na Kibilizi.

Lengo la mradi huoni kutatua mgogoro wa Wamiliki wa bajaji na daradara na kuiongezea manispaa mapato kutokana na kila bajaji kulipia shilingi 500 kwa kila siku endapo atatumia maegesho hayo kama ilivyo kusudiwa katika kikao cha Manispaa na SUMATRA.

Nae Afisa mfawidhi wa Mamlaka ya Usafiri wa nchi kavu na majini SUMATRA) Mkoani Kigoma, Bernad Marwa, alisema kanuni ya SUMATRA kwa Wamiliki wa vyombo vya usafiri yenye miguu miwili na mitatu wanatakiwa kujengewa maegesho watakayo kuwa wanasubili abilia hapo.

Kuhusiana na suala la kushusha abilia dereva atamshusha abilia mahali popote na kurudi katika kituo chake alicho pangiwa ilikusubili abiria wengine na watafanya kazi kama dereva tax wanavyo fanya haitakuwa kama walivyo kuwa wakifanya awali.

Alisema kwa atakaekiuka kanuni na taratibu zilizowekwa na SUMATRA atatakiwa kulipia shilingi 50,000 kama faini ya kukiuka taratibu zilikuweza.

No comments:

Powered by Blogger.