MWENYEKITI WA CCM KATA YA KAWEKAMO MANISPAA YA ILEMELA AANZA ZIARA YA KUIMARISHA CHAMA.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM, Kata ya Kawekamo Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza, Saad Rwekaka (Kulia), ameanza ziara ya Kukagua uhai wa Chama katika Kata hiyo.
Rwekaka alianza ziara hiyo April 02,206 katika tawi la CCM Msumbiji na baadae kuendelea katika Matawi mengine ambayo ni Pasiansi B ambapo ziara iliyofanyika April 09,2016, Apil 10,2016 katika tawi la Nyasaka A ambapo April 16 atakuwa katika tawi la Pasiansi Mashariki A na jumapili April 17 akiwa katika tawi la Nyasaka B.
Katika ziara zote hizo, Rwekaka anakutana na makundi yote ikiwemo makundi ya Wazee, Vijana, Mabalozi pamoja na Wanachama wa CCM katika Matawi ya Kata hiyo huku akijadiliana nao mikakati mbalimbali ya kuwashirikisha wananchi pamoja na kuisukuma Serikali ili kuweza kutatua changamoto zilizopo katika kata hiyo ikiwemo ubovu wa miundombinu ya barabara, ukosefu wa maji pamoja na hudumza za afya.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM, Kata ya Kawekamo Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza, Saad Rwekaka (Kushoto), akikabidhi zawadi za katiba za CCM kwa Neema Mapesa ambae ambae ni Katibu wa CCM Tawi la Pasiansi Mashariki B (Kulia), ikiwa ni ahadi aliyoitoa kwa tawi litakalotoa kura nyingi za CCM katika uchaguzi uliopita.
Consolatha Faustine ambae ni Katibu wa CCM Kata ya Kawekamo (aliesimama) akizungumza wakati wa ziara ya Mwenyekiti wa CCM katika Kata hiyo iliyofanyika katika Tawi la Pasiansi B.
Kutoka Kushoto waliokaa ni Paschal Bahindi ambae ni Katibu wa UVCCM Kata ya Kawekamo, Mwenyekiti wa CCM Kata ya Kawekamo na Katibu wa CCM Tawi la Pasiansi Mashariki B.
Viongozi na Wanachama wa Chama cha Mapinduzi Tawi la Pasiansi Mashariki B, Kata ya Kawekamo wakiwa katika mkutano na Mwenyekiti wa CCM katika Kata hiyo uliofanyika jumamosi April 9,2016.
Viongozi na Wanachama wa Chama cha Mapinduzi Tawi la Pasiansi Mashariki B, Kata ya Kawekamo wakiwa katika mkutano na Mwenyekiti wa CCM katika Kata hiyo uliofanyika jumamosi April 9,2016.
Imeandaliwa na George Binagi-GB Pazzo @BMG
No comments: