LIVE STREAM ADS

Header Ads

SHULE YA FUNGWA KWA KUKOSA VYOO NA MADAWAT

Na Rhoda Ezekiel, Kigoma
Shule ya msingi Kigogwe iliyopo kijiji cha Kigogwe Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma, inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa madawati na matundu ya vyoo kwa zaidi ya miaka 30 na hivyo kulazimika  shule hiyo kufungwa kwa muda hadi hapo huduma ya choo itakapopatikana.

Changamoto hizo imekuwa kero kwa wakazi hao pamoja na wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo,hali ambayo imewalazimu kuiomba serikali kuwatatulia kero hiyo licha ya wakazi wa kijiji hicho kuingilia kati na kuamua kuchimba matundu ya vyoo.

Mwalimu mkuu msaidizi wa shule hiyo Bikengela Tozwa na mwenyekiti wa kijiji hicho Habibu Bitwaye walisema hadi sasa kamati ya shule kwa kushirikiana na wananchi baada ya mkutano mkuu waliamua kujitolea kutekeleza jukumu hilo.

Aidha walisema wamekerwa na kitendo cha viongozi wao kuamua kufunga shule hiyo bila kuwashirikisha ambapo awali waliwashirikisha na kupitia ushirikishwaji huo wananchi waliamua kuchimba matundu sita ya vyoo katika shule hiyo jambo ambalo liliwatia hasira mara baada ya kuambiwa shule imefugwa.

Shule hiyo tambayo ilianza rasmi mwaka 1979 bado majengo yake ni tatizo lakini pia uhaba wa walimu ni tatizo ambapo walimu 26 wanahitajika, ukosefu wa madawati kwa darasa la kwanza, la pili na la tatu pamoja na darasa la awali kulazimika kukaa chini kwenye udongo, wengine wakikalia vigoda wakati wa masomo.

nae Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Merry Tesha , alisema tatizo hilo la upungufu wa madawati na ukosefu wa vyoo mashuleni ni tatizo sana katika wilaya  hiyo na tumejipanga kuhakikisha tutapambana nazo.

Tesha alisema tumeanza kutengeneza vyoo kwa baadhi ya  shule zilizo kuwa hazina vyoo na madawati yanaendelea kiutengenezwa iliifikapo mwezi wa sita mwishoni zoezi hilo liwe limekamilika.

"Tumejitahidi kuchangishana sisi kama viongozi wa Wilaya na baadhi ya wadau ilituweze kupambana na tatizo la upungufu wa madawati na tunamshukuru muheshimiwa Rais kwa mchango wake wa madawati mashuleni limeweza kupunguza tatizo hilo", alisma Tesha.

Shule hiyo inajumla ya wanafunzi 1158 na baadhi ya wanafunzi wa darasa la kwanza , la pili na la tatu wote wanalazimika kukaa chini kutokana na upungufu wa madawati.

No comments:

Powered by Blogger.