LIVE STREAM ADS

Header Ads

WAHITIMU WA MAHAFALI YA KWANZA KATIKA CHUO CHA UALIMU MOSHI WAAHIDIWA NEEMA.

Mgeni Rasmi, Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi CCM Taifa (UVCCM Taifa), Shaka Hamdu Shaka (wa pili kushoto), pamoja na viongozi wa chuo wakielekea ukumbini baada ya kuwasili katika eneo la Chuoni cha Ualimu "Moshi Teachers College" ikiwa ni katika Mahafali ya Kwanza ya Chuo hicho. 
Picha na Faradin Siraji 
Shaka aliwaasa wahitimu wa chuo hicho kutobweteka  baada ya masomo yao hivyo hivyo wajiendeleze zaidi kielimu ili kupanua wigo wao wa ajira. Wahitimu hao wametunukiwa vyeti ngazi ya cheti.

Katika mahafali hayo Shaka alitoa shilingi Milioni Moja ikiwa ni Mchango wake katika kuboresha baadhi ya miundombinu katika chuo hicho ambapo aliahidi kuwa bega kwa bega katika kuwasemea wahitimu hao ili Serikali iwapatie ajira kwa wakati na hivyo kupunguza tatizo la ajira kwa vijana pamoja na upungufu wa waalimu nchini.

Mahafali hayo yamefanyika wiki hii, ambapo Wahitimu 149 wametunukiwa vyeti vyao.

Mgeni rasmi pamoja na wageni wengine meza Kuu wakiimba Wakiimba nyimbo maalum ilioandaliwa na wahitimu.
Wanafunzi pamoja na familia zao Wakiwa ndani ya ukumbi tayari Kwa Shughuri nzima ya kutunukiwa vyeti kuanza.
Mwanafunzi Msoma Risala  akimkabidhi Mgeni Rasmi SHAKA HAMDU SHAKA risala hiyo.
Shaka Hamdu Shaka (Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa), aliwaasa wahitimu wa chuo hicho kutobweteka  baada ya masomo yao hivyo hivyo wajiendeleze zaidi kielimu ili kupanua wigo wao wa ajira. Wahitimu hao wametunukiwa vyeti ngazi ya cheti.

 Katika mahafali hayo Shaka alitoa shilingi Milioni Moja ikiwa ni Mchango wake katika kuboresha baadhi ya miundombinu katika chuo hicho ambapo aliahidi kuwa bega kwa bega katika kuwasemea wahitimu hao ili Serikali iwapatie ajira kwa wakati na hivyo kupunguza tatizo la ajira kwa vijana pamoja na upungufu wa waalimu nchini.
Mgeni Rasmi SHAKA HAMDU SHAKA (KAIMU KATIBU MKUU UVCCM TAIFA) akikabidhi vyeti kwa wahitimu

Mgeni Rasmi SHAKA HAMDU SHAKA (KAIMU KATIBU MKUU UVCCM TAIFA) akikabidhi vyeti kwa wahitimu
Wahitimu pamoja na Wazazi (Wageni waalikwa).
Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Chuo akizungumza katika mahafali hayo.
Miongoni mwa wahitimu 149 wa Chuo cha Ualimu Moshi. Ni katika Mahafali ya Kwanza ya Chuo hicho yaliyofanyika wiki hii.

No comments:

Powered by Blogger.