LIVE STREAM ADS

Header Ads

BEN PAUL ATIKISA KATIKA TAMASHA LA NYAMA CHOMA JIJINI DAR.


 Mwanamuziki mahiri  wa Rnb hapa nchini  , Bernard Michael Paul, maarufu kama ‘Ben Pol’ akitoa burudani  kwa maelfu ya wakazi wa Dar es salaam waliohudhuria maadhimisho ya miaka mitano ya  Tamasha la Nyama choma 2016.
Tigo ilimdhamini Ben Paul kutumbuiza katika tamasha hilo ambalo lilifanyika jumamosi katika viwanja vya Leaders.
Na Krantz Mwantepele


BEN POL akicheza na mashabiki zake jukwaani wakati wa tamasha la nyama choma katika viwanja vya leaders Jijini Dar es salaam 
Mashabikiwa muziki wa bongo fleva wakishangilia wakati Benpol anatumbuiza kibao chake cha MOYO MASHINE 
Benpol akihojiwa na mtangazaji wa Clouds fm Askofu Tza baada ya kutumbuiza katika tamasha la Nyama choma katika viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam.
Baadhi ya mawakala wa tigo waliokuwepo katika viwanja  vya Leaders kutoa msaada na huduma mbali mbali toka tigo ikiwemo huduma za intaneti ya kasi ya Tigo 4G LTE
Wakala wa tigo akisajili laini ya mteja katika tamasha la Nyama choma mapema jana usiku katika viwanja vya Leaders Jijini Dar es salaam.
Msanii mahiri wa Bongo fleva Vanessa Mdee akiongea jambo na mmoja wa shabiki zake katika viwanja  vya Leaders Jijini Dar es salaam
Mabanda ya tigo yaliyokuwepo uwanjani katika kutoa huduma mbalimbali kwa wateja wa tigo  waliofika katika tamasha la Nyama Choma 
Mmoja wa wapishi wa nyama akichoma nyama wakati wa tamasha la Nyama Choma katika viwanja vya leaders Jijini Dar es salaam.
Wadau wakiendelea kufurahia muziki na kula nyama choma katika tamasha liliofanyika mapema jana
Mmoja wa wakala wa Tigo akimsaidia mteja  kufungua intaneti ya tigo katika simu yake katika tamasha la Nyama Choma liliofanyika jumamosi usiku katika viwanja vya Leaders Jijini Dar es salaam.

No comments:

Powered by Blogger.