LIVE STREAM ADS

Header Ads

DIWANI WA KATA YA MABATINI JIJINI MWANZA AZINDUA KIKUNDI CHA USHIRIKIANO PEOPLE'S.

Diwani wa Kata ya Mabatini Jijini Mwanza, Deus Mbehe (Chadema) akikata utepe kama ishara ya Uzinduzi wa Kikundi cha Kusaidiana cha USHIRIKIANO PEOPLE'S kinachoundwa na Wanachama zaidi wa 100 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Kata ya Mabatini.
Na BMG

Kikundi hicho kiliundwa baada ya kuibuka stofahamu ya wananchi kusaidiana katika masuala mbalimbali ikiwemo misiba, baada ya baadhi ya wanachama wa chadema kutengwa katika shughuli za misiba katika Kata ya Mabatini.

Uzinduzi wa Kikundi hicho ulifanyika katika Ukumbi wa Kilimanjaro uliopo Mabatini Stand huku ukiambatana na harambee kwa ajili ya kukiimarisha kikundi ambapo diwani wa Kata ya Mabatini ambae alimwakilisha diwani wa Kata ya Butimba, akichangia shilingi Laki Tano huku wageni wengine waalikwa wakifanikisha harambee hiyo kufikisha shilingi Milioni Moja, laki moja na elfu sabini.

Wanachama nao waliahidi kila mmoja kuchangia shilingi elfu kumi, pesa ambazo kwa ujumla zitasaidia kukabiliana na mapungufu yanayokikabili kikundi hicho. Mapungufu hayo ni pamoja na viti 120, sufuria nne, turubai mbili pamoja na sahani 200 lengo likiwa ni kujiimarisha katika mahitaji mbalimbali yanayohitajika katika shughuli mbalimbali.

Mwenyekiti wa Kikundi hicho chenye wanachama 103 hadi sasa, Salma Ibrahim, amewasihi wananchi wengine kujiunga na kikundi ili kuongeza nguvu ya kusaidiana katika masuala mbalimbali ikiwemo sherehe, misiba na kuinuana kiuchumi bila kujali itikadi zao za kisiasa.
Kutoka Kushoto ni Mwenyekiti wa Chadema Kata ya Mbugani, Ibrahim Waryoba, Mwenyekiti wa Kikundi cha Ushirikiano People's, Salma Ibrahim, Diwani wa Kata ya Mabatini, Deus Mbehe, Mwenyekiti wa Mtaa wa Nyerere B, Mabatini, Therui Mtenga pamoja na Katibu wa Kikundi cha Ushirikiano People's, Abdallah Mkama.
Mwenyekiti wa Kikundi cha Ushirikiano People's, Salma Ibrahim, akizungumza katika uzinduzi wa kikundi hicho uliofanyika jana.
Diwani wa Kata ya Mabatini, Deus Mbehe, akizungumza katika uzinduzi wa Kikundi cha Ushirikiano People's cha Mabatini.
Diwani wa Kata ya Mabatini, Deus Mbehe, akizungumza katika uzinduzi wa Kikundi cha Ushirikiano People's cha Mabatini.
Diwani wa Kata ya Buzuruga, Richard Machemba, akizungumza katika uzinduzi wa Kikundi cha Ushirikiano People's cha Mabatini.
Katibu wa Kikundi cha Ushirikiano People's, Abdallah Mkama., akizungumza katika uzinduzi wa Kikundi cha Ushirikiano People's cha Mabatini.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Mabatini Kusini, Faridu Baltazary, akizungumza katika uzinduzi wa Kikundi cha Ushirikiano People's cha Mabatini. Wazo la kuasisiwa kwa Kikundi cha Ushirikiano People's liliibuka kutokana na mwenyekiti huyu kutengwa kutokana na itikadi za kisiasa baada ya kufiwa na mkewe.
Ndaisaba Aron kutoka Buzuruga, akizungumza katika uzinduzi wa Kikundi cha Ushirikiano People's cha Mabatini.
Florian Wabandi akisoma Risala ya Kikundi cha Ushirikiano People's mbele ya mgeni rasmi. Katika risala hiyo alisema kikundi hicho chenye lengo la kusaidiana katika shida na raha, kinakabiriwa na Mapungufu kadhaa ikiwemo viti 120, sufuria nne, turubai mbili pamoja na sahani 200 lengo likiwa ni kujiimarisha katika mahitaji mbalimbali yanayohitajika katika shughuli mbalimbali.
Mwenyekiti wa Kikundi cha Ushirikiano People's, Salma Ibrahim, akikabidhi risala ya kikundi kwa mgeni rasmi.
Mhasibu wa Kikundi akipongea mchango wa harambee kutoka kwa mgeni rasmi.
Wanachama wa Kikundi cha Ushirikiano People's kilichopo Mabatini Jijini Mwanza wakiwa katika uzinduzi wa Kikundi hicho uliofanyika jana.
Wanachama wa Kikundi cha Ushirikiano People's kilichopo Mabatini Jijini Mwanza wakimsikiliza kwa umakini mshereheshaji katika uzinduzi wa Kikundi hicho uliofanyika jana.
Wanachama wa Kikundi cha Ushirikiano People's kilichopo Mabatini Jijini Mwanza wakisalimiana kwa salamu ya people's power ya "Zungushaaaa" katika uzinduzi wa Kikundi hicho uliofanyika jana.
Wanachama wa Kikundi cha Ushirikiano People's kilichopo Mabatini Jijini Mwanza wakifurahia burudani katika uzinduzi wa Kikundi hicho uliofanyika jana.
Wanachama wa Kikundi cha Ushirikiano People's kilichopo Mabatini Jijini Mwanza wakifurahia burudani katika uzinduzi wa Kikundi hicho uliofanyika jana.
Mwenyekiti wa Kikundi cha Ushirikiano People's, Salma Ibrahim, akiongoza wageni waalikwa na wanachama kupata chakula katika uzinduzi rasmi wa kikundi hicho uliofanyika jana.
Wageni waalikwa na wakichukua chakula katika uzinduzi rasmi wa kikundi cha Ushirikiano People's uliofanyika jana.
Wageni waalikwa na wakichukua chakula katika uzinduzi rasmi wa kikundi cha Ushirikiano People's uliofanyika jana.

No comments:

Powered by Blogger.