LIVE STREAM ADS

Header Ads

BUNGE LAAHIRISHWA MJINI DODOMA BAADA YA HALI YA HEWA KUCHAFUKA.

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, limeahirisha shughuli zake za bunge hii leo (majira ya saa tano asubuhi).
Hatua hiyo imejiri baada ya wabunge kutaka kujadiliwa kwa hoja ya dharura ya mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nasari (chadema) juu ya suala la wanafunzi zaidi ya 700 wa diploma program maalumu kutoka chuo kikuu cha Dodoma waliokwama Dodoma baada ya kuambiwa warudi makwao hadi wanatakapoitwa tena.

Baada ya Mhe.Nasari kuwasilisha hoja hiyo, naibu spika Dkt.Tulia Ackson Mwansasu, alikataa kujadiliwa kwa hoja hiyo hali iliyosababisha baadhi ya wabunge wa pande zote (CCM na Ukawa) kuchafua hali ya hewa bungeni na hivyo kumlazimu naibu spika kulazimika kuahirisha bunge hilo hadi leo jioni.
Chanzo:Radio One Stereo

No comments:

Powered by Blogger.