LIVE STREAM ADS

Header Ads

JESHI LA POLISI MKOANI MWANZA LATOA KAULI YAKE JUU YA JEMBEKA FESTIVAL 2016.


Mkurugenzi wa Jembe Media Group, Dr.Sebastian Ndege, (kushoto) akiwa na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani kumkaribisha katika Tamasha kubwa la Jembeka Festival 2016 linalotarajiwa kufanyika Jumamosi Mei 21,2016 katika Uwanja wa CCM Kirumba.

Kamanda Msangi amewahakikishia usalama wa kutosha wakazi wa Jiji la Mwanza na watakaotoka nje ya Jiji la Mwanza katika tamasha hilo ambalo wasanii mbalimbali wanakiki watadondosha burudani babukubwa huku kubwa zaidi wakiwa ni Neyo kutoka Marekani pamoja na Diamond Platnumz kutoka Dar.

Dr.Ndege amemshukuru Kamanda Msangi kwa ushirikiano wake ambapo ameahidi kuhakikisha jamii inapata elimu juu ya usalama na utii wa sheria kupitia vyombo vyake vya habari ikiwemo Jembe Fm.

Katika tamasha hilo ambalo litafanyika katika Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza, viingilio itakuwa ni Shilingi 10,000, 50,000 na 100,000 hivyo huu ni muda wa kununua tiketi mapema mwana wa kwetu.

Imepewa nguvu na Vodacom Tanzania! Vodacom Kazi ni Kwako. Special Thanks FastJet, EF Outdoor, Mwananchi Communications,Samsung, Ndege Insurance, Syscorp Corporation, KK Security, JembeFm-JembeniJembe, Gsengo Blog, Binagi Blog, Michuzi Blog, Dj Choka, Lakairo Hotel na wadau wengine.

Mkurugenzi wa Jembe Media Group, Dr.Sebastian Ndege (kulia) akifurahia jambo na Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Miraji Mtaturu, baada ya kumtembelea ofisini kwake jana kumkaribisha kwenye Tamasha la Jembeka Festival 2016.
Picha na Gsengo Blog

No comments:

Powered by Blogger.