LIVE STREAM ADS

Header Ads

JUMUIYA YA WAZAZI WA CCM MKOANI KIGOMA YAIPIGA TAFU SHULE YA MSINGI NENGO ILIYOPO KIBONDO.

Na Rhoda Ezekiel, Kigoma.
Katika kuadhimisha wiki ya wazazi mkoani Kigoma, Jumuiya ya wazazi wa Chama cha Mapinduzi CCM, mkoani humo imetembelea shule ya msingi Nengo iliyopo Wilayani kibondo ambayo ni shule maalumu ya walemavu, ili kuchangia shughuli mbalimbali za maendeleo shuleni hapo.
                                  
Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo mkoani Kigoma, Nicholaus Zacharia amesema jumuiya imekabidhi mahitaji mbalimbali ikiwemo unga wa ugali, mchele, sukari, mafura ya kupikia na baloo la nguo za mitumba ambapo yote yamegharibu shilingi 1,200,000 ambazo zimetolewa na wanachama wa jumuiya hiyo kwa kushirikiana na Mbuge wa jimbo la Muhambwe.

Mkuu wa shule hiyo, Shabani Mzenzi, amewapongeza wazazi hao kwa kukumbuka mahitaji ya wanafunzi waliopo shuleni hapo ambapo amebainisha kwamba shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 616 ambapo wanafunzi 81 ni walemavu na 535 wakiwa hawana ulemavu.

No comments:

Powered by Blogger.