LIVE STREAM ADS

Header Ads

MAGONJWA HATARI YASIYOPEWA KIPAUMBELE SASA KUDHIBITIWA.


Judith Ferdinand na Getruda Ntakije, Mwanza
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto imeandaa mpango mkakati wa miaka mitano kwa ajili ya kudhibiti magonjwa yanayoisumbua jamii lakini hayapewi kipaumbele ikiwemo kichocho na minyoo ya tumbo.

Hayo yamesemwa jana na Katibu  Tawala Mkoa wa Mwanza, Kamishina Godwilg Mteve, katika kikao cha wafanyakazi  wa idara afya , kilichofanyika mkoani hapa.

" Utafiti unaonyesha ugonjwa wa kichocho umeenea zaidi kandokando ya Ziwa Victoria ambapo maambukizi yake ni asilimia 80 huku minyoo ya tumbo ikiwa asilimia 100," alisema Mteve.

Kaimu Mganga Mkuu Mkoa wa Mwanza, Dkt. Silas Wambura, alisema magonjwa hayo huleta mihangaiko na ulemavu kwa jamii, hali inayopunguza uwezo wa wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo sambamba na kupunguza mahudhurio ya watoto shuleni na kuathiri maendeleo ya masomo yao.

Naye Mratibu wa Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele Dkt. Mabai  Leonard alisema, wizara ikishirikiana na wadau mbalimbali, kutoa dawa mfululizo  kwa miaka mitano, kwa ajili ya  kukinga na kudhibiti ili baadae waweze kutokomeza magonjwa hayo.

No comments:

Powered by Blogger.