LIVE STREAM ADS

Header Ads

MAHAFALI YA KIDATO CHA SITA 2016, MKOLANI SEKONDARI JIJINI MWANZA YAFANA.

Jana Alhamisi, Mei 19,2016 ilikuwa ni siku yenye furaha kubwa kwa Wanafunzi wa Kidato cha Sita katika Shule ya Sekondari Mkolani iliyopo Jijini Mwanza ambapo walikuwa wakisherehekea Mahafali yao ya Kuhitimu kidato cha sita.

Mahafali hayo yalifanyika katika Ukumbi wa Shule hiyo, ambapo mgeni rasmi alikuwa ni diwani wa Kata ya Mkolani Mhe.Dismas Rithe. 
Pichani juu ni wahitimu hao ambao wamehitimu katika michepuo ya Sayansi (PCM, PCB, PGE) jumla yao ni 124, Wavulana wakiwa ni 14 na Wasichana wakiwa ni 110, wakiingia Ukumbini.

Akizungumza katika Mahafali hayo, Mkuu wa Shule hiyo, Mwalimu Asensio Mathias, alibainisha changamoto kadhaa zinazowakabiri wanafunzi shuleni hapo kuwa ni pamoja na upungufu wa waalimu wa masomo ya sayansi, vifaa vya maabara, madarasa, nyumba za waalimu pamoja na ukosefu wa uzio katika mabweni ya wasichana ambayo pia ni kwa ajili ya wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi wanaosoma katika shule hiyo na hivyo kuhatarisha usalama wao.

Mgeni Rasmi katika Mahafali hayo, Diwani wa Kata ya Mkolani, Mhe. Dismas Rithe, aliahidi kuwasilisha changamoto hizo katika ngazi husika ili kuzitafutia ufumbuzi.

Mwalimu Isaack Wakuganda akiendelea na shughuli yake ya shereheshaji katika Mahafali hayo.
Wahitimu wa Kidato cha Sita, Mkolani Sekondari ya Jijini Mwanza, wakiimba Wimbo wa Shule katika Mahafali yao yaliyofanyika jana shuleni hapo.
Wahitimu wa Kidato cha Sita, Mkolani Sekondari ya Jijini Mwanza, wakiimba Wimbo wa Shule katika Mahafali yao yaliyofanyika jana shuleni hapo.
Wahitimu wa Kidato cha Sita, Mkolani Sekondari ya Jijini Mwanza, wakiwa wameketi ikiwa ni katika Mahafali yao yaliyofanyika jana shuleni hapo.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Mkolani iliyopo Jijini Mwanza, Mwalimu Asensio Mathias akizungumza katika Mahafali ya nne ya Kidato cha Sita katika shule hiyo.
Mgeni rasmi katika Mahafali ya nne ya kidato cha Sita, Mkolani Sekondari Jijini Mwanza, ambae ni diwani wa Kata ya Mkolani Mhe.Dismas Rithe akizungumza katika Mahafali hayo.
Gervas Mtayangulwa ambae ni Mjumbe wa Bodi ya Shule, Mkolani Sekondari, akizungumza katika Mahafali ya nne ya Kidato cha Sita ya shule hiyo yaliyofanyika jana.
Wahitimu wa Kidato cha Sita, Mkolani Sekondari ya Jijini Mwanza, wakiimba wimbo wa kuwaaga wanafunzi wenzao wanaobaki shuleni hapo kuendelea na masomo.
Wanafunzi wenye ulemavu (mmoja ulemavu wa ngozi na mwingine ulemavu wa macho), wanaosoma katika Shule ya Sekondari Mkolani, wakiimba wimbo ambao uliwasisimua watu wengi ikiwa ni katika kuwaaga wahitimu wa kidato cha Sita katika shule hiyo kwenye Mahafali yaliyofanyika jana shuleni hapo.
Wahitimu wa Kidato cha Sita, Mkolani Sekondari 2016, wakisoma Risala yao
Taswira ukumbini katika Mahafali ya Kidato cha Sita, Mkolani Sekondari, ikiwaonesha Wazazi, Walezi, Waalimu, pamoja na Wanafunzi/ Wahitimu
 Wahitimu wa Kidato cha Sita wakionesha Umahiri wao katika Kucheza ngoza za Kisasa.
Wahitimu wa Kidato cha Sita wakionesha Umahiri wao katika Kucheza ngoza za Asili.
Mmoja wa Wahitimu wa Kidato cha Sita aliefanya vizuri katika masomo yake, Mkolani Sekondari akipokea Cheti ikiwa ni katika Mahafali ya nne ya kidato cha Sita shuleni hapo.
Mhitimu wa Kidato cha Sita aliefanya vizuri katika masomo yake, Mkolani Sekondari akipokea Cheti ikiwa ni katika Mahafali ya nne ya kidato cha Sita shuleni hapo.
Mmoja wa Wahitimu wa Kidato cha Sita aliefanya vizuri katika masomo yake, Mkolani Sekondari akipokea Cheti ikiwa ni katika Mahafali ya nne ya kidato cha Sita shuleni hapo.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Mkolani iliyopo Jijini Mwanza, Mwalimu Asensio Mathias, akiwa na logo ya 102.5 Lake Fm Mwanza.
Kushoto ni Martha Ernes na Kulia ni Consolatha Issack ambao ni miongoni mwa Wahitimu wa Kidato cha Sita 2016, Mkolani Sekondari, wakiwa na Logo ya 102.5 Lake Fm Mwanza katika Mahafali yao yaliyofanyika jana.
Irene Vicent ambae ni miongoni mwa Wahitimu wa Kidato cha Sita 2016, katika Shule ya Sekondari Mkolani akihojiwa na BMG.
Tazama HAPA Mahafali ya Kidato cha Sita Mwaka jana.
Imeandaliwa na BMG

No comments:

Powered by Blogger.