LIVE STREAM ADS

Header Ads

MKUU WA WILAYA YA UVINZA MKOANI KIGOMA ANG'AKA.


Na Rhoda Ezekiel, Kigoma
Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma, Mrisho Gambo amewaagiza Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo pamoja na watumishi wa vituo vya afya vya wialayani humo, kuacha kuwachangisha wananchi malipo ya  huduma za afya zilizotangazwa na Serikali kuwa kuwa zinatolewa bure.

Ametoa rai hiyo katika Kijiji cha Mazungwe kilichopo wilayani Uvinza wakati akizungumza na wananchi wa Kijiji hicho, katika eneo la ujenzi wa Zahanati ya Kijiji unaoendelea huku pia akijitambulisha kwa wadau wa maendeleo.

"Ni marufuku kuwachangisha wananchi gharama kwa ajili ya huduma za afya zilizotangazwa na serikali kuwa ni bure, na kama leo mngekuwa mmetozwa ningeamru hizo pesa zirudishwe".Amesema Gambo.

Wakitoa malalamiko yao mbele ya Mkuu huyo wa Wilaya, wananchi wa kijiji hicho wamesema wanasikitishwa na utaratibu wa wagonjwa kutozwa shilingi mia tatu ili waweze kupata huduma ya matibabu huku zahanati hiyo ikitoa huduma katika jengo bovu la nyasi pamoja na  kukosa dawa, vifaa tiba na upungufu wa watumishi.

Hata hivyo Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo, Dkt.Fani Mussa, amesema zipo huduma ambazo wananchi hawapaswi kulipia ikiwemo watoto chini ya miaka mitano kutibiwa bure ambapo amesisitiza kuwa ni marufuku watumishi wilayani Uvinza kuwaomba wananchi pesa kwa ajili ya matibabu katika huduma ambazo serikali imeagiza zitolewe bure.

No comments:

Powered by Blogger.