MWALIMU AFARIKI DUNIA KWA KUJINYONGA.
Na Rhoda Ezekiel, Kigoma
Mwalimu wa Shule ya Msingi Buzebazeba iliyopo katika Manispaa ya kigoma ujiji, ambae amefahamika kwa jina la Victoria Wiso (38), amefariki dunia baada ya kujinyonga akiwa nyumbani kwake.
Kamanda wa polisi Mkoani Kigoma ,ASCP Frednandi Mtui, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo ametanabaisha kwamba usiku marehemu alimuacha mmewe amelala na kuingia jikoni ambapo alijinyonga kwa kutumia kamba huku chanzo kilichompelekea kujinyonga kikiwa bado hakijafahamika.
Marehemu hajaacha ujumbe wowote na mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa Maweni kwa ajili ya uchunguzi zaidi kabla ya kwenda kuzikwa.
No comments: