LIVE STREAM ADS

Header Ads

DC KAHAMA AWATAKA MADIWANI KUTOKUBALI MAENEO YA VYANZO VYA MAJI KUUZWA.

Shaban Njia
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga, Vita Kawawa, amewataka Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Kahama kutokukubali kuuzwa kwa maeneo yaliotengwa kwa ajili ya hifadhi ya vyanzo vya ili kuunusuru mji huo na tatizo la ukosefu wa maji.

Kawawa alitoa angalizo hilo katika kikao cha Wadau wa Maji  kilichofanyika jana Mjini Kahama, kikiwa na lengo la kungalia changamoto inazoikabili Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Kahama na Shinyanga (KASHWASA) ambacho kiliwajumuisha pia Madiwani wa Halmashauri ya Kahama pamoja na Watendaji wa Kashwasa.

"Ninawaomba Madiwani wangu wa Halmashauri ya Mji wa Kahama msikubali kupitisha maombi ya  kuuza maeneo yenye Vyanzo vya maji  kama bwawa la Nyihogo katika Halmashauri yenu ili viweze kutumika kwa ajili ya matumizi ya shughuli za majumbani kwani kwa kufanya hivyo mtakuwa hamjawatendea haki wananchi wa Mji wa Kahama"Alisema Kawawa.

No comments:

Powered by Blogger.