LIVE STREAM ADS

Header Ads

WAKAZI WA KISIWA CHA GOZIBA WILAYA YA MLEBA MKOANI KAGERA WASHAURIWA KIJIKOMBOA.


Judith Ferdinand, Mwanza
Wakazi wa kisiwa cha Goziba, kilichopo wilayani Muleba mkoani Kagera, wametakiwa kuchangia na kushiriki katika shughuli  mbalimbali za kijaamii na maendeleo, ili kujikomboa kiuchumi.

Diwani wa Kata ya Goziba, Mhe.Mataba Nkunami, alitoa kauli hiyo jana na kuongeza kuwa kutokana na maeneo ya visiwa  kipindi cha nyuma kutumika katika shughuli za  uvuvi,na hayakuwa makazi ya kudumu tofauti na sasa, ndio sababu ya kukabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa zahanati, shule na maji salama.

Alisema wakazi wa maeneo ya visiwani  wanatakiwa kuchangia michango kwa namna yoyote, ili kuhakikiaha kunakuwepo na huduma za kijamii ikiwemo zahanati, shule pamoja na hupatikanaji wa maji safi na salama  kama ilivyo kwa maeneo mengine.

Pia aliiomba serikali  kutenga fedha kwa ajili ya kuboresha na kusaidia masuala mbalimbali katika maeneo ya visiwa ili maeneo hayo yaweze kukua kimaendeleo pamoja na kukuza uchumi wa taifa, kwa kuwa wananchi watafanya biashara na kutumia huduma ambazo watalazimika kulipa kodi.

No comments:

Powered by Blogger.