LIVE STREAM ADS

Header Ads

WANAFUNZI WASOMEA MSIKITINI MKOANI KIGOMA BAADA YA MTENDAJI KUTOWEKA NA FEDHA ZA UJENZI.


Na Rhoda Ezekiel, Kigoma
Wanafunzi wa shule ya msingi Nyantole iliyopo katika kijiji  cha Kigadye Mkoani Kigoma, wanalazimika kusomea katika msikiti uliopo katika kijiji hicho kutokana na shule hiyo kukosa madarasa ya kutosha baada ya aliyekuwa mtendaji wa kijiji hicho kutoweka na fedha za ujenzi katika shule hiyo kiasi cha 1,376,000.

Wakizungumza katika kikao cha Baraza la madiwani la Halmashauri ya Kigoma Vijijini, baadhi ya madiwani walimuomba Afisa utumishi wa Halmashauri hiyo kuwaeleza alichukua  hatua gani dhidi ya mtendaji aliye isababishia serikali hasara ya Wanafunzi kukosa  madarasa.

Zuberi mafutaa ambae ni diwani wa kata ya Ziwani alisema  aliyekuwa mtendaji wa kijiji cha Kigadye, Daudi Sugwejo, aliondoka kijijini hapo na fedha za serikali ya kijiji ikiwemo fedha zilizo tengwa kwa ajiri ya ujenzi wa madarasa ya shule hiyo  na kusababisha Shule hiyo kukosa madarasa.

Kaimu Afisa utumishi wa Halmashauri ya Kigoma Vijijini, Fubusa Ruhanga, alisema "tulipokea tuhuma kutoka kwa viongozi wa kijiji cha kigadye zinazo mtuhumu kuondoka na pesa hizo na tukampa  hati ya mashtaka na siku 14  ili aweze kujibu tuhuma zinazomkabili.

Katika utetezi wake, mtendaji huyo alisema kwamba alipohamishwa alikabidhi vifaa vyote na fedha kiasi cha shilingi 2,000,000/=  kwa kamati ya ujenzi mnamo tarehe 03/12/2015 mbele ya mashahidi Haidhuru Haruna, Ahmad Mussa na Majaliwa Said ambae alikuwa mwenyekiti wa kamati ya ujenzi kijijini hapo.  

Alisema ofisi yake inapitia utetezi huo na vielelezo alivyowasilisha kabla ya kuunda kamati ya uchunguzi juu ya suala hilo ili hatua za kinidhamu zichukuliwe dhidi ya mtuhumiwa ikiwa atapatikana na hatia ikiwemo kurejesha fedha hizo.

No comments:

Powered by Blogger.