LIVE STREAM ADS

Header Ads

HONGERA TCRA KWA KUZIMA SIMU FAKE JAPO KAZI BADO IPO.


Kwa wale watumiaji wa simu zisizo halali (Simu Fake), haya ndiyo yaliyowasibu kuanzia usiku wa kuamkia leo. Kumbuka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA, ilitangaza kuzima simu zisizo halali (fake) June 16,2016 kuanzia saa 23:59 Usiku.


Hata hivyo zoezi hilo licha ya kufanikiwa kwa baadhi ya simu, pia baadhi ya simu zenye chipu (line) mbili zimekumbwa na sintofahamu kwani simu nyingine zimeonekana mtandao kusoma chipu moja huku chipu ya pili ikiwa haisomi. 

Pia kwenye suala la kutumia huduma ya Internet kwa njia ya Wi-Fi, bado huduma hiyo inapatikana kwa simu "fake" ambazo mawasiliano yake mengine kama kupiga na kupokea simu hayapatikani.

BMG tunasema hakuna mafanikio yasiyo na changamoto hivyo hongera TCRA kwa kuthubutu kulinda afya za watumiaji wa simu nchini Tanzania, kwani simu "fake" zina madhara mengi kiafya, lakini kazi bado ni pevu hivyo juhudi zaidi ziendelee kufanyika ili kuhakikisha zoezi hili linafanikiwa zaidi bila kujali kelele zinazopigwa mitaani kwa wanaoendeleza matumizi ya simu zisizo halali (fake).

No comments:

Powered by Blogger.