LIVE STREAM ADS

Header Ads

IPO NGUVU YA MUNGU KATIKA MKUTANO MKUBWA WA INJILI "OYES 2016" UNAOFANYIKA JIJINI MWANZA.

Mchungaji wa Kanisa la "EAGT Lumala Mpya International Church", Dr.Daniel Moses Kulola, akifanya maombezi kwa wahitaji mbalimbali ikiwemo wagonjwa katika Mkutano  Mkubwa wa Injili wa Open Your Eyes and See OYES 2016 ulioanza unaofanyika katika viwanja vya kanisa hilo vilivyopo Sabasaba Manispaa ya Ilemela Jijini Mwanza.

Mkutano huo ulianza jumapili iliyopita June 12 na unatarajia kufikia tamati kesho kutwa jumapili june 19 hivyo hakikisha haukosi kufika katika mkutano huo maana ipo nguvu ya Mungu na wenye vifungo mbalimbali wamefunguliwa tangu kuanza kwa mkutano huo.

Mwimbaji na Mhubiri JJ.Rwiza, akihubiri katika Mkutano wa OYES 2016
Mwimbaji na Mhubiri JJ.Rwiza, akifanya maombezi katika Mkutano wa OYES 2016
Waimba wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya wakihudumu katika Mkutano wa OYES 2016.

No comments:

Powered by Blogger.