LIVE STREAM ADS

Header Ads

JINSI MKUTANO WA INJILI WA REINHARD BONNKE ULIVYOHITIMISHWA KWA SHANGWE JIJINI MWANZA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Nasi Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Mkutano Mkubwa wa Injili wa Reinhard Bonnke, Uliokuwa Ukihubiriwa na Mhubiri wa Kimataifa kutoka nchini Ujerumani, Daniel Kolenda (Kulia), jana umefikitia tamati huku maelfu ya waumini na wakazi wa Jiji la Mwanza wakihudhuria mkutano huo kwa siku zote tangu Alhamisi June 23,2016 hadi tamati jana June 26,2016.

Mkutano huo ambao ulikuwa ukifanyika katika Uwanja wa Furahisha, uliandaliwa chini ya Huduma ya Injili ya Christ For All Nations kwa kushirikiana na Umoja wa Makanisa Jijini Mwanza. Watu wengi walipokea muujiza wa Kristo huku wengine wakisalimisha tunguri zao walizokuwa wakitumia katika ushirikina ambapo ziliteketekwa katika mkutano huo.
Na BMG
Daniel Kolenda (kulia) akihubiri katika Mkutano huo jana. Katikati ni mtumishi wa Mungu Askofu Eugen Mulisa wa Kanisa la HHC Alive la Jijini Mwanza, akitafsiri mahubiri hayo kwa lugha ya kiswahili.
Askofu Eugen Mulisa (katikati) wa Kanisa la HHC Alive la Jijini Mwanza, akitafsiri mahubiri ya Daniel Kolenda (kulia) kutoka lugha ya Kiingereza kwenda katika Kiswahili.
Maelfu ya Waumini wa dini mbalimbali pamoja na Wakazi wa Jiji la Mwanza, wakiwa katika Mkutano huo.

No comments:

Powered by Blogger.