LIVE STREAM ADS

Header Ads

KAMATI YA MAWASILIANO MKOA WA MWANZA YATOA ELIMU KWA WATUMIAJI WA HUDUMA ZA MAWASILIANO.

Mwenyekiti wa Kamati ya Mawasiliano Mkoa wa Mwanza, Jonathan Abdallah Kasibu, akizungumza katika Semina kwa Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Jijini Mwanza iliyofanyika jana katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Mwanza.

Katika semina hiyo, watumiaji wa hudumza za mawasiliano ikiwemo simu pamoja na vyombo vya habari ambao waliwakilisha makundi mbalimbali kama vile wanahabari, wajasiriamali na walemavu, walipewa elimu juu ya uwepo wa Kamati hiyo pamoja na uwepo wa Baraza la Ushauri la Watumiaji wa huduma za Mawasiliano kutoka Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA-CCC).

Pia walielimishwa juu ya mwongozo wa kuwasilisha malalamiko ya watumiaji wa huduma za mawasiliano, haki na wajibu wa mtumiaji wa huduma za mawasiliano pamoja na sheria ya makosa ya mitandao ya mwaka 2015.

Semina hiyo pia ilihudhuriwa na viongozi wa Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano, kutoka Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA-CCC) ambapo iliambatana na viongozi wa Kamati ya Mawasiliano mkoani Mwanza kujitambulisha kwa baraza hilo.

Watumiaji wa huduma za mawasiliano walielezwa kwamba ni wajibu wao kuwasilisha malalamiko yao ikiwa wanapokea huduma zilizo chini ya kiwango ama ikiwa wana malalamiko ya aina yoyote kuhusu huduma za mawasiliano.

Walihimizwa kuwasilisha malalamiko yao kwa kuanza na mtoa huduma, yasiposhughulikiwa wanawayawasilisha katika Kamati ya Huduma za Mawasiliano mkoa, yasipotatuliwa yatawasilishwa katika Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano kutoka TCRA na hata ngazi nyingine zaidi hadi pale utatuzi utakapofanyika.

Semina hiyo ilionekana kuwafungua ufahamu watumiaji wa huduma za mawasiliano jijini Mwanza kwani baadhi yao walieleza kuwa awali walikuwa hawatambui haki na wajibu wao katika kutumia huduma za mawasiliano.
Katikati ni Katibu wa Kamati ya Mawasiliano mkoani Mwanza, Jimmy Luhende, akitoa mada katika semina hiyo.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano kutoka Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA-CCC), akizungumza katika semina hiyo.
Kushoto ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano kutoka Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA-CCC), akijitambulisha katika semina hiyo. Kulia ni mjumbe wa Baraza hilo, Salma Abdallah.
Baadhi ya Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Jijini Mwanza, wakiwa katika semina ya kuwaelimisha juu ya Matumizi ya Huduma za Mawasiliano.
Imeandaliwa na BMG

No comments:

Powered by Blogger.