LIVE STREAM ADS

Header Ads

MCHUNGAJI WA KIMATAIFA MAMA DOMITILA NABIBONE KUTOKA NCHINI CANADA AWASILI JIJINI MWANZA KWA AJILI YA MKUTANO WA OYES 2016.

Ujumbe wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo Sabasaba Manisapaa ya Ilemela mkoani Mwanza, ukiongozwa na Mchungaji wa Kanisa hilo Dkt.Daniel Moses Kulola (Wa Pili Kushoto), ukiwa katika Uwanja wa ndege Jijini Mwanza kwa ajili ya kumpokea Mhubiri wa Kimataifa kutoka nchini Canada Mama Domitila Nabibone (Wa tatu kushoto) aliefika Jijini Mwanza kwa ajili ya Mkutano Mkubwa wa Open Your Eyes and See (OYES 2016) unaofanyika katika Kanisa hilo.

Wa kwanza kushoto ni Mama Mchungaji, Mercy Kulola pamoja na waumini wengine wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya wakiwemo Wazee wa Kanisa. Mkutano wa OYES 2016 ulianza jana June 12,2016 katika viwanja vya Kanisa hilo na unatarajia kufikia tamati jumapili ijayo June 19,2016 ambapo kila siku utakuwa ukianza majira ya saa nane mchana.

Mchungaji Mama Nabibone anazo shuhuda mbalimbali ikiwemo kuwaapisha Sara ya Toba zaidi ya Marais wanne duniani huku kubwa zaidi ikiwa ni kufufuka siku ya nne baada ya kufariki. Hakika usikose kufika katika Mkutano wa OYES 2016.
Mhubiri wa Kimataifa kutoka nchini Canada Mama Domitila Nabibone (katikati) akipokelewa jana jijini Mwanza kwa ajili ya Mkutano wa OYES 2016.
Mhubiri wa Kimataifa kutoka nchini Canada Mama Domitila Nabibone, akipokelewa jijini Mwanza.
Mhubiri wa Kimataifa kutoka nchini Canada Mama Domitila Nabibone, akipokelewa jijini Mwanza.

No comments:

Powered by Blogger.