WAKALI WA ACTION MOVIE BONGO, JPLUS NA INSPECTOR SEBA WAKUTANA TENA.
J.Plus (Kushoto) & Inspector Seba (Kulia).
Nyota wa filamu za Action nchini Tanzania ambaye ni mmoja
kati ya waasisi wa filamu hizo, Jimmy Mponda maarufu kama “J.Plus” aliyeanza
rasimi kutoa Action Muvi ya “Shamba kubwa” mnamo mwaka 1994, Filamu yake ya
pili ikafuata 1995, ilipewa jina la “Unga Adui” yatatu iliitwa “Kifo haramu”
ilikuwa 1997 ya nne ilikuwa “Usia” 2003.
2005-2010 Jplus na
Seba walienea kwenye masikio ya watu baada ya kutoa filamu ya “Misukosuko”
iliyo dumu kwa muda wa miaka 5 bila kupoteza ubora wake kwenye masikio ya
mashabiki. 2012 Jplus alitoa filamu ya “Double. J” ambayo tunaweza kusema ilikuwa
kama filam yake ya mwisho kwa maana ya kwamba toka kipindi hicho J.plus hajatoa
filamu yeyote mpaka hii leo.
Refere: 2005 ilipotoka filamu ya “Misukosuko” kulikuwa na
mgawanyiko wa mashakiki yaani kama team
za mpira, Mashabiki wa “J.Plus” na Mashabiki wa Sebastian Mwanangulo maarufu
kama “Inspector Seba” kutokana na mpambano wao katika muvi hiyo, Baada ya Part
1 na Part 2 kuisha Scene za “Seba” hazikuwepo tena ingawa Misukosuko iliendelea
na Part zingine.
Hali hiyo ilipelekea wadau mbalimbali wa filamu kudhani kuwa
wawili hao huenda wakawa labda waliingia kwenye mgogoro, lakini hakukua majibu
ya uhakika yaliyo bainika kama kweli J.Plus na Seba walitofautiana kauli.
Baada ya Kimya cha miaka 3 iliyopita nyota wa filamu hizo za
Action “J.Plus” kupitia ‘Mzimuni Theatre Arts’ anategemea kuvunja ukimya 2016
kwa kuja upya na filamu mpya ya ‘The Foundation’ ( Msingi) ambayo kwa upande
wake J.plus amesema “Nategemea hii
filamu ya ‘The Foundation’ irudishe heshima ya Muvi za Action Tanzania kama
ilivyo kuwa awali.
Hivyo wadau wangu na fans wang ambao walikuwa wanatamani
kuona J.Plus na Seba wakicheza Filamu moja basi huu ni ujio mpya wenye kasi
kubwa ‘The Foundation’ imechezwa na Jimmy Mponda a.k.a J.Plus, Sebastian Mwanangulo a.k.a Inspector Seba,
Christina Aidan, Saidi Ndomboroa, Mariamu Mustafa, OP Mohamed a.ka Guga,
Ramadhani Mohamed a.k.a Junior nk. Hivyo Staytuned, mtaarifu na mwenzio
naomba mapokezi mema kutoka kwenu
watanzania thanks.”
No comments: