WCF YAWAFIKIA MADAKTARI 380 IKIJIANDAA KUANZA KUTOA FIDIA JULAI MOSI MWAKA HUU.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, Masha Mshomba, akitoa hotuba kwenye
ufunguzi wa mafunzo ya siku tano kwa madaktari kutoka mikoa ya Nyanda za Juu
Kusini, ambapo mafunzo hayo yalianza jana june 3,206 mkoani Mbeya.
Mafunzo hayo ni muendelezo wa kampeni ya WCF kwa kushirikiana na Shirika la Kazi Duniani, ILO, kuwapatia mafunzo Madaktari kote nchini, ili kujenga uwezowa kufanya tathmini ya madhara aliyoyapata mfanyakazimahala pa kazi kabla ya kupatiwa fidia. WCF itaanza kutoa Fidia kwa Wafanyakazi Kuanzia Julai 1, 2016.
PICHA ZOTE NA EMMANULE MADAFA
Mafunzo hayo ni muendelezo wa kampeni ya WCF kwa kushirikiana na Shirika la Kazi Duniani, ILO, kuwapatia mafunzo Madaktari kote nchini, ili kujenga uwezowa kufanya tathmini ya madhara aliyoyapata mfanyakazimahala pa kazi kabla ya kupatiwa fidia. WCF itaanza kutoa Fidia kwa Wafanyakazi Kuanzia Julai 1, 2016.
PICHA ZOTE NA EMMANULE MADAFA
Baadhi ya madaktari waliohudhuria mafunzo hayo
KATIBU
Tawala Wilaya ya Mbeya, Bi.Quip G. Mbeyela(pichani juu), amefungua mafunzo kwa madaktari
kutoka kanda ya Nyanda za Juu Kusini katika ukumbi wa Tughimbe Jijini Mbeya na kutoa rai kwa Mfuko wa Fidia kwa Wanyakazi kuhakikisha
wanawashindanisha madaktari wote waliopewa mafunzo kuhusu ajali na magonjwa
yanayotokana na kazi ili wale madaktari wataofanya vizuri waweze kupewa
motisha.
Mfuko
wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), kwa kushirikiana na Wataalamu kutoka Shirika
la Kazi Duniani, (ILO), imetoa mafunzo ka madaktari wapatao 380 kutoka katika
hospitali za rufaa mikoani na wilayani Tanzania Bara. Zoezi hili limefanyika
katika vituo vikumbwa vinne ikiwemo Dar es salaam, Arusha, Mwanza na kumalizia
na Jiji la Mbeya linalohusisha madaktari kutoka mikoa na halmashauri za Mbeya,
Songwe, Rukwa, Iringa, Njombe, Ruvuma na Katavi.
Mwakilishi
wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya fedha na
uwekezaji ya Bodi Dkt. Francis Michael, ametoa shukrani za dhati kwa Serikali kwa uamuzi wa
kuanzisha mpango thabiti wa kushughulikia masuala ya fidia pale wafanyakazi
wanapoumia au kupata magonjwa kazini. Aidha, shukrani zangu pia ziufikie
uongozi wa serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais wetu John Pombe Magufuli kwa
kuwajali wafanyakazi wake, ambapo tayari kiasi cha asilimia 0.5% ya mshahara wa kila Mfanyakazi wa Umma kimeshatengwa
kupitia makadirio ya mapato na matumizi ya serikali kwa mwaka wa fedha
2016/2017.
Nae Mkurugenzi Mkuu amesema Mfuko wa
Fidia kwa Wafanyakazi, utatoa Huduma na Mafao Bora ikiwemo huduma ya matibabu,
malipo ya ulemavu wa muda, malipo ya ulemavu wa kudumu, malipo kwa
anayemhudumia mgonjwa, huduma za ukarabati na ushauri nasaha pamoja na malipo
kwa wategemezi endapo mfanyakazi atafariki akiwa anatekeleza majukumu ya
mwajiri wake.
Mfuko
wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) uko mbioni kuanza malipo ya fidia ifikapo tarehe
01 Julai 2016. Wanufaika na fidia itakayotolewa ni wafanyakazi wote Tanzania
Bara walio katika sekta binafsi na sekta ya umma watakaoumia, kuugua ama
kufariki kutoka na kazi.
Picha ya pamoja ya uongozi wa mkoa wa Mbeya, viongozi wa WCF, Wataalamu wa ILO na madaktari
Wataalamu wa ILO, (Kushoto) na Viongozi wa WCF
No comments: