LIVE STREAM ADS

Header Ads

ASWEKWA RUMANDE JIJINI MWANZA KWA KOSA LA KUMTUSI RAIS MAGUFULI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Ahmed Msangi, akizungumza na Wanahabari (picha kutoka maktaba).
Na BMG

Kijana mmoja Jijini Mwanza, amejikuta katika hali ya utata baada ya wenzake kumfikisha polisi kwa kosa la kumtukana Rais Dkt.John Pombe Magufuli.

Duru za habari zinaeleza kwamba, kijana huyo akiwa na wenzake aliomba lifti kwenye gari moja aina ya Noah, akiwa ndani ya gari hilo akasema kitendo cha kuomba lifti kimetokana na ugumu wa maisha uliosababishwa na Rais Magufuli aliemuita jina lisilo la kimaadili la...msh***i.

BMG inaendelea kumtafuta Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Ahmed Msangi, ili kuzungumzia tukio hilo, kwani alipopigiwa simu muda mfupi uliopita, simu yake ilipokelewa na dereva ambae aliedokeza kwamba Kamanda Msangi yuko kwenye kikao.

No comments:

Powered by Blogger.