CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO CHADEMA, KUIBUKA NA KAMPENI MPYA YA UKUTA.
Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA
MAENDELEO (CHADEMA) MAAZIMIO YA KIKAO CHA KAMATI KUU ILIYOFANYIKA HOTELI YA BAHARI BEACH
LEDGER PLAZA, 23-26 JULAI, 2016
1.0 UTANGULIZI
Kamati Kuu ya dharura ya Chama iliketi kuanzia tarehe 23-26 Julai, 2016 Jijini Dar Es Salaam
na ilikuwa na ajenda moja mahsusi ambayo ni kujadili
hali ya siasa na uchumi wa Taifa tangu serikali ya awamu ya tano
ilipoingia madarakani mwezi Novemba, 2015.
Mwenendo wa serikali hii ya CCM ya awamu ya tano, chini ya Rais John Magufuli, ni dhahiri
kuwa umeamua kuiweka demokrasia kizuizini na kuleta utawala wa Kidikteta katika
nchi yetu.
2.0 MATUKIO MAHSUSI YA UKANDAMIZAJI WA HAKI NA DEMOKRASIA NCHINI
2.1 Kupiga Marufuku Mikutano ya Vyama vya Siasa: Serikali kupitia Waziri Mkuu na
hatimaye Rais na jeshi la Polisi walitangaza kwa nyakati tofauti kwamba ni marufuku kwa vyama vya
siasa kufanya mikutano ya kisiasa mpaka
mwaka 2020 ili kuipa Serikali nafasi ya kufanya kazi. Huu ni uvunjaji wa
Ibara ya 20 (1) ya Katiba.
Aidha, katazo la mikutano ya siasa linakiuka Sheria namba 5 ya Vyama vya siasa ya mwaka
1992 kifungu cha 11 ambayo imetoa haki kwa vyama
vya siasa kufanya kazi ya siasa.
2.2 Kupiga Marufuku Urushwaji wa moja kwa moja (live coverage) wa Mijadala ya Bunge: Katazo hilo ni
kinyume na Katiba ibara ya 18 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo inatoa
uhuru wa maoni na uhuru wa kupata habari kwa
kila mwananchi.
2.3 Kudhibiti Wabunge wa Upinzani Bungeni: Serikali imejificha nyuma ya kiti cha Naibu
Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson Mwansasu (Mb)
ili kuwadhibiti Wabunge wa Upinzani Bungeni kwa lengo la kuwanyamazisha wasiikosoe Serikali.
Ikumbukwe
kwamba Dkt. Tulia akiwa Naibu Mwanasheria
Mkuu wa Serikali alikuwa ni mtumishi wa umma asiyepaswa kuwa mwanachama wa
chama chochote cha siasa; lakini ghafla
anaonekana akigombea nafasi ya Naibu Spika kupitia
CCM. Hivyo yupo Naibu Spika ambaye ni mteule wa Rais. Swali: Anawajibika
kwa nani kati ya Bunge na Rais?
2.4 Kuingilia Mhimili wa Mahakama: Serikali ya CCM kupitia Rais, kwa nyakati tofauti
imeonekana kujaribu kuingilia uhuru wa Mahakama
jambo ambalo ni hatari kwa utoaji wa haki nchini.
Katika hotuba yake,
wakati wa maadhimisho ya siku ya sheria
duniani Rais alinukuliwa akisema kwamba
Mahakama iwahukumu harakaharaka watu waliokwepa kodi halafu
atatumia asilimia fulani ya fedha ambazo
zitakuwa zimepatikana kutokana na faini
za wale walioshindwa kesi kuwapa Mahakama.
2.5 Kupuuza Utawala wa Sheria: Tarehe 24 Juni, 2016 wakati wa
uzinduzi wa siku ya
usalama wa raia, Rais Magufuli alinukuliwa akiwaruhusu polisi kuwaua majambazi bila
kuwafikisha mahakamani ili sheria ichukue
mkondo wake. Aidha aliuagiza uongozi wa Jeshi la Polisi
kuwapandisha vyeo watakaowauwa majambazi.
2.6 Muswada wa Sheria ya Haki ya kupata habari –Serikali imepeleka Bungeni Muswada
wa Sheria ya Haki ya kupata habari. Sheria
hii imeweka adhabu kubwa sana kwa waandishi kama vile kifungo cha miaka
15 na kisichozidi miaka 20 kwa mujibu
wa kifungu cha 6(6)
2.7 Serikali hii inatishia ukuaji wa uchumi Tangu serikali ilipoingia madarakani
hali ya ukuaji wa uchumi na hata
uwekezaji wa mitaji imekuwa ikiporomoka kwa kasi kubwa sana nchini
mwetu na hata baadhi ya wawekezaji wanaondoa
mitaji yao kutokana na serikali hii kukosa mwelekeo unaoeleweka wa Kiuchumi.
2.8 Serikali za mitaa kunyanganywa mapato na serikali kuu. Baada
ya uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 tulifanikiwa kushinda
maeneo ya Majiji ya DSM, Mbeya,Arusha na Miji mikubwa ya Iringa,
Moshi,Bukoba,Babati,Tunduma na mingineyo ya maeneo
ya mijini ambayo kwa kiasi kikubwa wanategemea sana kuendesha Halimashauri hizo kwa kutumia
kodi ya Majengo Kodi ya Majengo inachangia
kati ya 30% hadi 60% ya mapato ya ndani ya Mamlaka za Miji.
2.9 Diplomasia na
mahusiano ya kimataifa Hivi karibuni serikali imetoa maelekezo
kupitia mawasiliano yake na Mabalozi (Note Verbale)
kuelekeza kuwa kabla ya Mabalozi au maofisa
wa Ubalozi kukutana na asasi zisizo za kiserikali au vyama vya siasa ni
lazima kwanza waombe kibali cha serikali kupitia
Wizara ya Mambo Nje.
Utaratibu huu unaminya uhuru wa mabalozi na wanadiplomasia
mbalimbali kufanya kazi zao
nchini na ni utaratibu ambao unakiuka utamaduni uliokuwepo
awali na pia unakiuka masharti ya Mkataba wa Vienna kuhusu mahusiano
ya Kibalozi Duniani.
2.10 Uteuzi wa Wakurugenzi
wa Halimashauri Uteuzi wa Rais wa Wakurugenzi wa Halimashauri na Makatibu Tawala wa Wilaya haukuzingatia
sheria za utumishi wa umma na badala yake
umezingatia kigezo cha Ukada zaidi badala ya weledi na historia katika
utumishi wa umma kama ambavyo sheria zinataka,
zaidi ya wakurugenzi 80 na Makatibu tawala
zaidi ya 40 waligombea kura za maoni ndani ya CCM 2015.
2.11 ZANZIBAR
Kwa sababu ya hasira ya kukataliwa kwa CCM, vikosi vya ulinzi na hasa Jeshi la Polisi vimekuwa
vikishiriki katika vitendo kadhaa vya ukiukwaji
wa haki za raia huko Zanzibar ambapo kwa zaidi ya miezi miwili sasa,
wamekuwa wakipita katika vijiji na kuwapiga, kuwatesa,
kuwakamata, kuwatishia na hata kuharibu mali za wananchi na mifugo yao .
Tunawataka wananchi wa Unguja na Pemba
waendelee kuikataa Serikali haramu iliyopo
madarakani huko Zanzibar kwa njia za amani .
3.0 MAAZIMIO YA KAMATI KUU
Baada ya majadiliano Kamati Kuu imeazimia ifuatavyo;
3.1 Septemba 1, siku ya
mikutano ya hadhara nchi nzima Kamati kuu imeagiza ngazi zote za chama
kuanzia ngazi ya msingi, Kata,
Majimbo, Wilaya, Mikoa, Kanda, Mabaraza na Taifa kukaa vikao
vyake vya kikatiba na imeelekeza ajenda ya
vikao hivyo kuwa ni kujadili hali ya siasa, hali ya uchumi na maandalizi ya
mikutano ya hadhara ya tarehe 01 Septemba, 2016
nchi nzima.
3.2 Wanasheria wa Chama
kuchukua hatua Kamati Kuu imewataka wanasheria wa chama kukaa
na kuyatazama mambo yote ambayo yametokea
na kuchukua hatua za kisheria kwa lengo la kuyatafutia suluhisho la kisheria.
3.3 OPERESHENI UKUTA
UMOJA WA KUPAMBANA NA UDIKTETA TANZANIA (UKUTA)
UTANGULIZI
Kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika
utangulizi kuna maneno
yameandikwa na ambayo yamekaziwa na sheria namba 15 ya mwaka 1984 ibara ya 3 na sheria namba 1 ya mwaka 2005
ibara ya 3. Katika utangulizi huo wa katiba yetu
imeandikwa kama ifuatayavyo;
“KWA KUWA Sisi wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
tumeamua rasmi na kwa
dhati kujenga katika nchi yetu jamii inayozingatia misingi ya uhuru, haki, udugu
na amani”
“NA KWA KUWA misingi hiyo yaweza tu
kutekelezwa katika jamii yenye demokrasia,
ambayo Serikali yake husimamiwa na Bunge lenye wajumbe
waliochaguliwa na linalowawakilisha
wananchi na pia yenye Mahakama huru zinazotekeleza wajibu wa kutoa haki bila woga wala upendeleo wowote
na hivyo kuhakikisha kwamba haki zote za
binadamu zinadumishwa na kulindwa na wajibu wa kila mtu
unatekelezwa kwa uaminifu:”
“KWA HIYO, BASI, KATIBA HII IMETUNGWA NA BUNGE MAALUM LA JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA kwa niaba ya
Wananchi kwa madhumuni ya kujenga jamii
kama hiyo na pia kwa ajili ya kuhakikisha kwamba Tanzania
inaongozwa na Serikali yenye kufuata
misingi ya Demokrasia ujamaa na isiyokuwa na Dini”
Aidha kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzana ibara
ya 3 (1) inasema kuwa
“Jamhuri ya Muungano ni Nchi ya Kidemokrasia na ya kijamaa, isiyokuwa na dini, yenye kufuata mfumo wa vyama vingi vya
siasa”
Ni wazi sasa kuwa kuna tishio kubwa dhidi ya ukuaji wa Demokrasia
hapa Nchini mwetu kutoka
kwa viongozi wa serikali hii ya awamu ya tano kukandamiza Demokrasia na madhara ya kukandamizwa kwa demokrasia
yameshaanza kulitafuna taifa letu.
Ni dhahiri kuwa kama raia wema tuna wajibu na haki ya kuilinda na
kuitetea Katiba ya Nchi
na kuhakikisha kuwa haivunji na yeyote na misingi ya Kidemokrasia ambayo ilijengwa kwa miongo mingi inaendelea
kuimarika, kulelewa na kukuzwa mara dufu.
3. 4 KWANINI UKUTA NI MUHIMU !
Wakati wa Ufashisti wa Adolf Hitler huko Ujerumani unaanza
kuchipua kabla ya kukomaa alianza
kuchukua hatua mbalimbali za kuwanyamazisha Wajerumani kwa njia mbalimbali ili aweze kutawala kwa mkono wa Chuma.
Alikuwepo Mchungaji mmoja anayejulikana kwa jina la Martin
Niemoller na ambaye alikuwa
akimsemea Hitler kwa kila hatua ambazo alikuwa anachukua dhidi ya makundi mengine katika jamii ya wajerumani
bila kujua kuwa lilikuwa ni suala la muda tu kabla hata yeye hajafikiwa na mkono wa Chuma
wa Hitler.
Mchungaji huyu ni maarufu sana kwa msemo wake ambao aliutoa
alipofikiwa na mkono wa
Hitler ambao ulimpelekea kuishia jela kwa miaka 7 na wakati huo hapakuwa na mtetezi wa kumsemea, alisema hivi;
First they came for the Socialists, and I did not speak out—Because
I was not a Socialist.
Then they came for the Trade Unionists, and I did not speak out—Because
I was not a Trade Unionist.
Then they came for the Jews, and I did not speak out—Because I was
not a Jew.
Then they came for me—and there was no one left to speak for me.
3.5 HALI TANZANIA IKOJE?
Tangu utawala wa awamu ya Tano ulipoingia madarakani mwezi
Novemba, 2015 umechukua hatua mbalimbali za kubinya
Demokrasia na kuua dhana ya utawala bora
kwa njia mbalimbali.
Yapo makundi ya kijamii ambayo tayari yameshaumizwa au kubinywa na
watanzania walio wengi wanakaa kimya kwa sababu
wao sio sehemu ya kundi husika ambalo
limenyimwa haki au kwa kuwa hajafikiwa moja kwa moja.
3.6 KWANINI NI MUHIMU KUJENGA UKUTA.
·
Rais alipiga
marufuku safari za nje kwa watumishi wa umma- sikusema kwa kuwa mimi sikuwa
mtumishi wa umma.
·
Rais aliitaka
mahakama kuu iwahukumu wafanyabiashara ambao wana kesi za kodi na serikali
lazima ishinde-sikusema kwa kuwa sikuwa mfanyabiashara na wala sikuwa na kesi
ya kodi.
·
Serikali
iliingilia Bunge na kupanga kamati za kudumu za Bunge-sikusema kwa kuwa mimi
sikuwa mjumbe.
·
Serikali ilizuia
matangazo ya Bunge live-sikusema kwa kuwa mimi sio Mbunge.
·
Wabunge wa
Upinzani kunyanyaswa Bungeni na kuonewa –sikusema kwa kuwa mimi sio UKAWA.
·
Hotuba za
Upinzani kufutwa Bungeni kinyume cha Kanuni za Bunge –sikuwa mpinzani nilikaa
kimya.
·
Bunge kurejesha
fedha zake kwa Rais kinyume cha sheria –sikusema kwa kuwa halinihusu.
·
Tume ya Taifa ya
Uchaguzi kurejesha fedha kwa Rais kinyume cha sheria – sikusema kwa kuwa Tume
hainihusu.
·
Serikali
Kuwafukuza na kuwadhalilisha wanafunzi wa UDOM –sikusema kwa kuwa sina ndugu
wala mtoto anayesoma UDOM.
·
Mikutano ya
kisiasa kupigwa Marufuku –sikusema kwa kuwa mimi sio mwanasiasa.
·
Wafanyabiashara
kupelekewa bili kubwa za kodi na hata kuzuiliwa kwa Akaunti zao-sikusema kwa kuwa
mimi sio mfanyabiashara.
·
Uchumi
unaporomoka kwenye sekta zote nchini -sikusema kwa kuwa mimi sijawahi kumiliki
uchumi.
·
Fao la kujitoa
limeondolewa kwenye Mifuko ya hifadhi ya jamii, sikusema kwa sababu mimi si
mwanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii.
·
Mashirika na
Makampuni kuanza kupunguza wafanyakazi kutokana na kuporomoka kwa uchumi
–sikusema kwa kuwa sijapunguzwa kazini.
·
Mabalozi na
wanadiplomasia kuzuiliwa kukutana na viongozi wa kisiasa bila kibali cha
serikali- sikusema kwa kuwa halinihusu.
·
Watumishi wa umma
kulazimishwa kwenda kinyume na sheria na kanuni za utumishi wa umma wametakiwa
kuwa Makada wa CCM –sikusema kwa kuwa mimi sio mtumishi wa umma.
·
Ukaguzi wa vyeti
vya kidato cha nne na kutumika kama msingi wa kufukuza watu kazi hata kama ni
Maprofesa –sikusema kwa kuwa hawajaja kwenye sekta yangu.
·
Watumishi wa umma
kutumbuliwa majipu bila kufuatwa kwa sheria na kanuni za utumishi wa umma
–sikusema kwa kuwa mimi sikutumbuliwa.
·
Mawakili
kuunganishwa kwenye kesi za wateja wao wanapoenda kuwatetea –sikusema kwa kuwa
mimi sio wakili.
·
Waalimu kukatwa
mishahara iwapo dawati litavunjika kwenye shule yake –sikusema kwa kuwa mimi
sio mwalimu.
·
Kupotezwa kwa
wana CCM ambao watapinga kauli ya Mwenyekiti au kuwa namaoni tofauti-sikusema
kwa kuwa mimi sio mjumbe wa vikao vya CCM .
·
Muswada wa sheria
ya haki ya kupata habari na adhabu ya kifungo cha miaka 15-20- sikusema kwa
kuwa mimi sio mwandishi wa habari.
·
Viongozi wa dini
kudhalilishwa –sikusema kwa kuwa mimi sio kiongozi wa dini.
·
Unyanyasaji na
udhalilishaji wa wananchi Zanzibar –sikusema kwa kuwa mimi sio mzanzibari.
3.7 TUCHUKUE HATUA!
i. Kwa kuwa wewe tayari umeshafikiwa hauna budi kujenga UKUTA ili
kuzuia wengine wasidhurike na utawala huu.
ii. Kwa kuwa wewe hujafikiwa na ndio maana husemi wenzako
wanapofikiwa, njoo tujenge UKUTA ili ukifikiwa awepo wa kusema
iii. Tuungane Tujenge UKUTA ili kuzuia uchumi wetu kuporomoka
iv. Njoo Tujenge UKUTA kuzuia Udikteta huu
v. Tujenge UKUTA tuilinde Katiba yetu
vi. UKUTA huu ni wa wananchi wote bila kujali dini, kabila, chama
cha siasa au rangi.
Historia inaonyesha kuwa Duniani pote Hakuna utawala uliwahi
kuushinda UKUTA wa wananchi .Na hii ndio Nguvu ya Umma. Kila mmoja achukue hatua
popote alipo ya kujenga UKUTA!
Imetolewa na;
Freeman A Mbowe
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa
27 Julai, 2016
No comments: