LIVE STREAM ADS

Header Ads

ILIVYOKUWA KATIKA HUKUMU YA KESI YA MAUAJI YA MWANAHABARI DAUD MWANGOSI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Daud Mwangosi, Enzi za Uhai wake.
Na BMG


Mahakama Kuu Kanda ya Iringa, leo imemhukumu jela miaka 15 askari, Pasificus Cleofas Simon, kutokana na kesi ya mauaji ya aliekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoani Iringa, Daud Mwangosi iliyokuwa ikimkabiri.

Askari Simon alikuwa akikabiriwa na kesi ya mauaji ya bila kukusudia, yaliyotokea Septemba 02,2012 katika Kijiji cha Nyololo mkoani Iringa ambapo marehemu Mwangosi alikuwa akitekeleza majukumu yake kama mwandishi wa Chanel Ten.

Tukio hilo lilitokea wakati wa mkutano wa kisiasa wa Chadema ambao hata hivyo awali ulikuwa umezuiliwa na jeshi la polisi mkoani Iringa usifanyike ambapo katika harakati za polisi kuuzuia kwa kutumia mabomu ya machozi, kitu kinachodhaniwa kuwa ni bomu la machozi kutoka kwa askari Simon, kilimlipukia Mwangosi akiwa mikononi mwa polisi na kupoteza maisha papo hapo.

Jaji Mkuu wa Mahakama Kuu Kanda ya Iringa, Paul Kiwelo, ametanabaisha kwamba hukumu hiyo imetolewa baada ya mashauriano baina ya pande zote mbili za upande wa Jamhuri na Utetezi kukamilika ambapo askari Simon alipatikana na kesi ya kuua bila kukusudia.
Askari Simon (mwenye kofia nyekundu) akiwasili mahakamani wakati wa usikilizwaji wa kesi.

Siku zote za kesi hiyo, mwenendo wa kesi ulikuwa na wakati mgumu hususani kwa waandishi wa habari ambapo walikuwa wakishindwa hata kumpiga picha kutokana na ulinzi mkali uliokuwa ukitanda wakati mtuhumiwa akifikishwa mahakamani na hata wakati wa kutoka mahakamani, tofauti na watuhumiwa wengine hali ambayo ilikuwa likizua maswali mengine kadhaa.
Habari na Picha zote, Kwa Hisani ya Mtandao.

No comments:

Powered by Blogger.