LIVE STREAM ADS

Header Ads

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUTOKA TDL.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Meneja Masoko na Udhaamini wa Kampuni ya TBL, George Kavishe, akizungumza na Wanahabari katika Uzinduzi wa Motisha Mpya Nunua, Uza, Shinda na Konyagi kwa Wasambazaji wa kinywaji cha Konyagi Kanda ya Ziwa ambao ulifanyika Julai 21,2016 Jijini Mwanza.

Mwanza – Julai 21, 2016: Kampuni ya Tanzania Distilleriers Limited (TDL) inayotengeneza na kusambaza kinywaji maarufu cha Konyagi na jamii zake, leo imezindua rasmi kampeni ya NUNUA, UZA, SHINDA NA KONYAGI kwa wasambazaji wa bidhaa zake itakayodumu kwa muda wa wiki 12.

Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni hiyo iliyofanyika katika Hotel ya Protea Oystebay - Dar es salaam, Mwakilishi wa Kampuni ya TDL, Meneja Masoko na Udhamini  Bwana George Kavishe alisema; 

“Dhumuni kuu la kampuni yetu ya TDL kuzindua kampeni ni kwanza kabisa kuwainua wasambazaji wa biashara zetu. Tutaweza kufikia lengo hili kwani washindi wa kampeni hii watajishidia magari mapya mawili ya usambazaji (Eicher 3 Tonne Truck zenye dhamani yazaidi ya milioni 90). Tunaamini kwa magari haya wasambazaji wetu wataweza kurahisishwa utendaji wao ndani ya maeneo yao ya mauzo”.

Pia, kupitia shindano hili tutaweza kuchangia maendeleo ya kichumi nchini pamoja na jamii kwa ujumla. Aliendelea kusema.
Naye Meneja wa Chapa ya Konyagi Bi Martha Bangu alisema;

“Katika shindano hili wasambazaji wa bidhaa zetu wamewekewa viwango vya mauzo; na washiriki wote watakaofikia vigezo wataingia kwenye droo kubwa ya kupata mshindi itakayofayika mwanzoni mwa mwezi wa 10. Tunaamini kabisa kampeni hii itaongeza ufanisi kwa wasambazaji wetu nao watoongezea chachu ya manunuzi ya bidhaa zetu”.
MWISHO

Kuhusu TBL Group:
TBL Group ni kampuni tanzu ya kampuni ya SABMiller.TBL Group inajumuisha makampuni ya Tanzania Breweries Ltd (TBL),Tanzania Distilleries Ltd (TDL) na DarBrew Limited. 

TBL Group imeorodheshwa katika Soko la Hisa la Dar es alaam,imeajiri wafanyakazi  2145  nchini Tanzania. Inaendesha viwanda 4 vya kutengeneza bia ,viwanda 3 vya vinywaji vya asili,kiwanda cha vinywaji vikali na mvinyo,kiwanda cha kusindika kimea na vituo vikubwa kumi vya usambazaji bidhaa zake nchini kote.

Vinywaji maarufu vinavyotengenezwa na kampuni ya TBL Group ambavyo vinatamba kwenye masoko nchini ni Safari Lager, Kilimanjaro Premium Lager, Ndovu Special Malt, Castle Lite, Castle Lager, Castle Milk Stout, Redd’s Original, Balimi Extra Lager, Eagle Lager, Eagle Dark, Grand Malt na Safari Sparkling Water. Vingine ni Konyagi, Zanzi Cream Liqueur, Dodoma Wine, Chibuku Super, Chibuku Shake Shake na  Nzagamba.

TBL imeshinda tuzo mbalimbali nchini baadhi yake zikiwa ni Tuzo ya Mwajiri bora mwaka (2015),Tuzo ya mzalishaji bora (2015) na imetangazwa kuwa mlipa kodi bora nchini kwa kipindi cha miaka 4 mfululizo

Kwa maelezo zaidi tafadhali wasiliana na: Mkurugenzi wa Masuala ya Kampuni - Georgia Mutagahywa kupitia   barua pepe hii: georgia.mutagahywa@tz.sabmiller.com
Bonyeza HAPA Kutazama Picha

No comments:

Powered by Blogger.