LIVE STREAM ADS

Header Ads

JIWE LA GIZANI KWA WANA-SIMBA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Wana Simba kesho watafanya kosa kubwa sana katika historia ya timu yao kama wataamua kumnyima timu Mo Dewji.

Unaposema Billion 20, ndogo je nani anatoa zaidi ya hapo au nani amewahi kutoa zaidi ya hapo na je ipi thamani ya Simba??
Ukitoa ukubwa wa jina la Simba hakuna kingine cha ziada, yale majengo mawili pale Msimbazi yenye rangi za kupauka na lile pori kule Bunju havifiki Bilioni 20.

Wanasimba watuambie ni lini timu yao imewahi kuwa na mtaji wa Bilioni 20?? Au baada ya miaka mingapi kuanzia sasa Simba watakua wametengeneza Bilion 20.

Wana Simba wacheni mapenzi ya kijinga, nini maana ya timu ya wanachama isiyokua na maendeleo, timu isiyoweza kupambana na mpinzani wake mkuu kwenye soko la usajili. Leo hii ukiona mchezaji mzuri kasajiliwa Simba, basi jua Yanga hawajamtaka,

Na ukiona mchezaji mzuri anachezea Simba kipindi hiki basi jua Yanga hawamtaki. Ilipofikia Yanga sasa hivi inaweza kuchukua mchezaji yoyote kutoka Simba, aliwahi kusema Manji naweza kuchukua wachezaji wa Simba wote wakawa wanafanya mazoezi Coco huku nawalipa mshahara bila kucheza ligi, kwa kauli hiyo hakuna hata kiongozi wa Simba aliethubutu kumjibu.

Simba mnapata wapi Mashaka na Mo, kama mliweza kumwamini Aveva ambae wakati anagombea hakua na sera yoyote zaidi ya kunyoosha vidole vitatu akiashiria point 3 ambazo pia zimemshinda mnashindwaje kumwamini Mo.

Katika watu wote wanaogombea uongozi Simba kila mmoja anasema ataongeza mapato ya klabu lakini hawasemi wataongeza vipi na wataongeza kiasi gani, sana sana watakimbilia kusema watauza jezi na kusimamia kodi za majengo ya msimbazi.

Lakini Mo amesema ataongeza kufikia bilioni 5 kwa Mwaka, na ameelezea itaongezekaje, Simba mnataka nini???
Siku moja Rage akiwa Rais nilikutana nae Posta katika ofisi za Bunge akiwa na bahasha mkononi, akanionyesha hela ndani ya bahasha hiyo ( kiasi nimesahau) akaniambia hizi pesa nimepewa na sasa hivi na Hans Pope nipeleke timu Angola kurudiana na Libolo, hizo zilikuwa pesa binafsi za Pope.

Siku nyingiine tena, nikiwa nyumbani kwa Rage akampigia simu Mbunge Profesa Maji Marefu, akamuomba hela ya sikumbuki ya nini lakini ilikuwa ni kwa matumizi ya Simba.

Hayo maisha yamepitwa na wakati, wana Simba msione mambo yanaenda ndani ya klabu yenu mkajua hali ni shwari ukweli ni kuwa viongozi wenu wanaomba omba. Tajiri mnaemuaminia Hans Pope mara ngap amesikika akilia njaa Simba, mnashindwa kumsajili mchezaji kutoka nchi masikini zaidi Afrika (Burundi)!!!

Mnashindwa akili na Yanga, wao wamemuuzia Manji timu bure.
Ndio Manji kanunua Yanga bure, na Yanga hawahoji kwa kua timu yao inapata ushindi.

Mwanachama gani Yanga anajua thamani ya mkataba wa Yanga na Quality Group, lini tenda ilitangazwa kwa makampuni kubid kugombania kuidhamini Yanga, Hakuna kilichofanyika hata kimoja, tumeamka na kuiona Yanga inavaa jezi za mdhamini Mpya.
Hata kamati ya utendaji ya Yanga haiwezi furukuta kwa sababu Yanga ni ya Manji, wao wamechagulia kwa matakwa ya katiba tu lakini hawana cha kuhoji kwa Manji.

Kama Manji kapewa timu bure, nyie mnashindwaje kumpa Mo kwa bilioni 20. Tena Mo yuko smart enough, anasema licha ya yeye kuwa na hisa kubwa lakini atashawishi wadhamini wengine waingie Simba.

Cheki Manji anachowafanyia Yanga, katimua wadhamini akiwemo TBL, Azam Tv lakini Mo atawaalika wadhamini wengine.
Simba amkeni kuna wajanja wanamkataa Mo kwa faida yao, wanataka wapate elfu 10 wakati wa uchaguzi. Simba mnataka nini tena?? Mnashindwaje kumuamini mtu anaendesha biashara zaidi ya 100.

Waingereza hawawapendi waarabu haswa waislamu lakini alivyokuja Sheikh Mansour hawakujali yote hayo wakamuuzia Manchester City kiulaini, nyie Simba mnapata wapi kigugumizi???.
Nimalize kwa kusema, tunakoelekea makampuni mengi yatashindwa kudhamini timu maana Magufuli kawabana kwenye kodi sasa Simba msiposhtuka mapema itakula kwenu kwa kutegemea ndo ndo ndo za wadhamini.

Niseme tuu mkinyima timu Mo mtakua mmefanya ujinga wa kiwango cha PHD....
Na Ahmed Ally, Mwandishi wa Habari za Michezo Tz.

No comments:

Powered by Blogger.