LIVE STREAM ADS

Header Ads

KARAMA ZA ROHONI NA MCHUNGAJI DANIEL KULOLA WA EAGT LUMALA MPYA INTERNATIONAL CHURCH.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Mchungaji Dkt.Daniel Moses Kulola (mwenye suti) wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya Internationa Church lililopo Sabasaba Ilemela Jijini Mwanza, akiwa katika ibada ya kusifu pamoja na waumini wa Kanisa hilo.
Na BMG
Mchungaji Dkt.Daniel Moses Kulola anatufundisha somo juu ya Karama za Rohoni. Anasema Karama za Rohoni ni matunda yaliyo moyoni mwa mtu/mwanadamu alieokoka. Ni upendo, furaha na matendo mema.

Ni matunda yanayoturahisishia safari yetu ya mbinguni. Ni upendo unaokuunganisha wewe ulieokoka na Yesu Kristo. Dkt.Kulola anasema wakati mwingine katika maisha ya mwanadamu kuna wasaa ambao pesa na mali ulizonazo haziwezi kukusaidia, badala yake unahitaji upendo wa kweli kutoka kwa Yesu Kristo.

Hivyo kabla hujadai upendo huo kutoka kwa Yesu, unapaswa kwanza wewe uwe na upendo huo (Upendo wa dhati) kama wa Yesu, kwa wanadamu wenzako kwani bila kuwa na upendo wa kweli (karama ya rohoni) ni ngumu kuwa karibu na Roho Mtakatifu ambae ni mwokozi wa maisha yako.

Kuwa na karama za rohoni kunakuepusha na mitego ya ibirisi. Ukiwa na karama za rohoni utaweza kuyashinda magumu yote yaliyo mbele yako. Zingatia karama zako ili uwe karibu na Kristo.

Rejea katika maandiko matakatifu ili kuimarisha zaidi karama zako za rohoni; Wagalatia 5:22, 1-Wakorintho 12:5-10, Yohana 3:16

No comments:

Powered by Blogger.