LIVE STREAM ADS

Header Ads

LIJUE SOKO KUBWA LA KIMATAIFA LA ROCK CITY MALL LILILOPO JIJINI MWANZA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

BMG imebaini kwamba Rock City Mall ni soko la Kimataifa kubwa kuliko yote Afrika Mashariki. Soko hili lina ukubwa wa mita za mraba 48,250 huku likiwa na eneo la maegesho ya magari 600, pikipiki na baiskeli 150, eneo la michezo ya watoto mita za mraba 15,200 na hivyo kufanya eneo lote la Rock City Mall kuwa mita za mraba 71,990.

Soko la Rock City Mall linafuatiwa na Soko la Mlimani City lililopo Jijini Dar es salaam lenye mita za mraba 11,500 ambalo ni soko kubwa Afrika Mashariki lililochukua nafasi ya pili kwa ukubwa baada ya lile la nchini Kenya la Westgate kuvamiwa. Westgate ilikuwa na ukubwa wa mita za mraba 30,000.

Ukifika Rock City Mall utafurahi kupata kila aina ya mahitaji pamoja na michezo ya watoto. Pia kuna huduma na maduka ya kila aina na bado uwekezaji unaendelea kufanyika. Lakini kwa waandaaji wa matamasha hapa ndipo mahali pake. 

Hakika Jiji la Mwanza (Ilemela na Nyamagana) pamoja na Mfuko wa Pensheni wa Serikali za Mitaa (LAPF), wanastahili pongezi kwa kufanikisha mradi huu mkubwa. 
Tazama baadhi ya Mandhari ya ndani ya Rock City Mall.
Kila mmoja busy ndani ya Rock City Mall
Mdau
Baada ya mahemezi, baadhi yao hufanya utalii wa ndani kidogo
Wadau wa BMG
Kila mtu busy ndani ya Rock City Mall

No comments:

Powered by Blogger.