LIVE STREAM ADS

Header Ads

WAKALA WA MISITU WILAYANI KAHAMA ASAIDIA KUMALIZA TATIZO LA MADAWATI KATIKA WILAYA HIYO.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Na Shaban Njia
Wakala wa Misitu katika Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga (TFS), imetoa magogo 360 na mbao 391 kwa ajili ya utengezaji wa madawati hali ambayo itasaidia kutatua upungu wa madawati katika mkoa wa shinyanga.

Kaimu Meneja  wa misitu, Mohamed Dossa, aliyasema hayo jana na kubainisha kwamba katika kukabiliana na changamoto ya uhaba wa madawati ambao upo katika maeneo mbalimbali nchini, wakala huo umeamua kutoa magogo na mbao katika halmashauri nne za mkoa wa shinyanga ambazo bado zinaupungufu mkubwa wa madawati.

Alisema kuwa pamoja na utoaji wa magogo hayo pia wametoa mbao 391 katika halmashauri tatu zilizopo wilayani Kahama  ambapo halmashauri ya mji wa Kahama ilipatiwa mbao 122, halmashauri ya Msalala mbao 146 pamoja na halmashauri ya Ushetu iliyopatiwa mabo 123.

Nae Esther Jesephat ambae ni afisa mistu wilayani Kahama, aliwataka wananchi wanaoishi kuzunguka katika maeneo ya misitu kuwa mabalozi wema kwa kutoa taarifa za uharibifu wa misitu hali itakayosaidia kupunguza uharibifu wa misitu.

No comments:

Powered by Blogger.