LIVE STREAM ADS

Header Ads

NAFASI YA KIBALI KATIKA MAFANIKIO YAKO.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Na George Binagi-GB Pazzo
Baadhi ya watu hushindwa kufikia malengo yao kwa sababu ya kukosa Kibali. Kibali ambacho hakichelewi wala hakiwahi. Kibali ambacho huja kwa wakati. Si kibali kutoka kwa mwanadamu bali ni Kibali kutoka kwa Mwenyezi Mungi, mwingi wa Rehema.

Haijalishi wewe ni mchapa kazi kiasi gani, kikubwa usikate tamaa. Waweza kuwa bora kwa kila hali ila ukashindwa kufikia malengo yako ikiwemo kukosa ajira nk.

Usikate tamaa bali ngojea kibali chako ili utusue maishani. Fanya kazi kwa bidii ili kibali kikija utishe zaidi kimafanikio.

Si kwamba #BMG ni bora zaidi kuliko #BMG za wengine. Ni kwa sababu tu imepata kibali kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Kibali chako chaja, kuwa mbunifu, piga kazi, UTAFANIKIWA.

Kumbuka #Kibali ni #Neema ya kukubalika kwa
Mungu, Wazazi, Walezi ama Watu tofauti tofauti maishani mwako.

Neno la Mungu linatuambia, "Basi Mungu alimjalia Daniel kupata #Kibali na huruma machoni pa huyo mkuu wa matowashi". Rejea kitabu cha Daniel 1:9 na kuendelea.

Ndugu yangu, tafuta #Kibali ili ufikie mafanikio yako. Na ili kupata #Kibali ni vyema ukawa na Bidii, Utiifu, Uaminifu, Unyenyekevu na Roho ya kumcha Mungu ikiwa ni miongoni mwa matendo mengi uyajuayo ambayo yanampendeza Mungu. 
Ungana nami kila siku kupitia #Binagi_Blog #BMG

No comments:

Powered by Blogger.