LIVE STREAM ADS

Header Ads

NAIBU WAZIRI WA MICHEZO APIGA MARUFUKU USHURU KATIKA MASUALA YA KIMICHEZO.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Na Shaban Njia
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni, Sana na Michezo, Anastazia Wambura, amepiga marufuku halmashauri zote nchi kutoza fedha za Ushuru katika shughuli zote za kijamii zinazofanyika kwa maslahi ya wananchi hususani katika masula ya michezo.

Wambura aliyasema hayo juzi katika kilele cha mbio za baiskeli zilizofanyika Mjini Kahama na kuhusisha washiriki kutoka  mikoa sita iliyopo kanda ya ziwa maarufu kama “Acacia tufanikiwe pamoja” iliyofadhiliwa na Kampuni ya Uchimbaji dhahabu ya acacia chini ya Migodi yake mitatu ya Buzwagi, North Mara pamoja na Bulyanhulu.

Alisema kuwa kitendo cha halmashauri ya Mji wa Kahama kuwatoza Ushuru Wawekezaji hao kwa ajili ya uwanja wa halmashauri na mambo mengine ni kinyume na utaratibu kwa mashindano hayo yalikuwa yakihusu jamii na sii taasisi yeyote ile.

Mwenyekiti wa Chama cha Baiskeli nchini (CHABATA) Godfrey Mhagama, alisemakuwa chama chake kilikuwa kimefunga mkataba wa miaka mitatu na kampuni ya Acacia juu ya mashindano ya baiskeli ya Kanda ya ziwa na mwaka huu ndio wa mwisho na kuwataka wawekezaji hao kuangalia kama kutakuwa na uwezekano wa kuongeza udhamini wao.

Nae Meneja Mkuu wa mgodi wa Buzwagi, Asa Mwaipopo, alisema kuwa lengo la mashindano hayoni kukuza vipaji vya waendesha baiskel na kuongeza kuwa hapa nchini kuna vipaji vingi ambavyo vimejifika hali ambayo kwa sasa hawana budi kuviibua na hasa kwa njia ya mashindano kama hayo ya baiskeli.

Katika mashindano hayo yaliyoshirikisha waendesha baiskeli kutoka katika mikoa ya Shinyanga, Mwanza, Kagera, Simiyu Geita na Mara yalijumuisha wanaume pamoja na wanawake ambapo wanaume walikimbia umbali wa kilometa 156 wakati wanawake walikimbia umbali wa kilometa 80.

Washindi katika mashindano wa upande wa wanaume alikuwa ni Seni Konda kutoka Shinyanga aliyepata kikombe na fedha tasilimu shilingi milioni moja na nusu,wapili alikuwa Makoja Khamisi kutoka Shinyanga aliyepata shilingi miliuoni moja na watatu alikuwa Charles Clemence aliyepata laki saba.

Kwa upande wa wanawake mshindi wa kwanza alikuwa Martha Anthon kutoka Mwanza  aliyepatakikombe na fedha tasilimu milioni moja na lakimbili,Mshindi wa pili alikuwa Selina Wiliam kutoka Geita aliyepata zawadi ya shilingi laki nane wakati mshindi wa tatu alikuwa Elizabeth Clement aliyepata kiasi cha shilingi laki sita.
Tazama HAPA Picha

No comments:

Powered by Blogger.