LIVE STREAM ADS

Header Ads

RAIS MAGUFULI KUFANYA ZIARA YA KWANZA MKOANI SINGIDA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com


Rais Magufuli.
Na Mathias Canal, Singida
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Pombe Magufuli, anatarajiwa kufanya ziara ya kwanza mkoani Singida tangu achaguliwe kuwa Rais wa awamu ya tano ikiwa pia ni ziara ya kwanza tangu achaguliwe kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM.

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida, Miraji Jumanne Mtaturu, ameyasema hayo wakati akitoa taarifa ya ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli anayetaraji kuwasili Mkoani humo tarehe 29 mwezi huu.

Rais Magufuli atafanya ziara ya katika Wilaya hiyo Mkoani humo ambapo kabla ya kuwasili Wilayani Ikungi atazuru Wilayani Manyoni akitokea Mkoani Dodoma.

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida.
Rais Magufuli yupo katika Chereko ya kumbukumbu nzuri ya ushindi wa asilimia mia moja aliyoipata mwishoni mwa juma wakati akikabidhiwa kijiti cha kuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa na wajumbe wote wa chama hicho.

Hii ni ziara yake ya kwanza kuzuru mkoani Singida tangu alipochaguliwa kuwa Rais wa Awamu ya tano Octoba mwaka Jana na tangu awe Kiongozi mkuu wa Chama Cha Mapinduzi.

No comments:

Powered by Blogger.