LIVE STREAM ADS

Header Ads

SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUTOKA OJADACT NA UTPC BAADA YA KIFO CHA MKUU WA VIPINDI BARMEDAS TV MWANZA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Salamu za rambirambi zimeendelea kutolewa kwa ndugu, jamaa na marafiki wakiwemo Waandishi wa Habari mkoani Mwanza, baada ya kifo cha aliekuwa Mkuu wa Vipindi Barmedas Tv, Mwalimu Charles Sokoro (pichani), aliefariki dunia jumamosi Julai 16,2016 saa mbili usiku katika Hospitali ya Rufaa Bugando alikokuwa amelazwa.

Salamu kutoka UTPC
Naomba mnifikishie salam zangu za rambirambi kwa ndugu na Jamaa pamoja na waandishi wa Mwanza, kwa ujumla nimepokea kwa mshtuko mkubwa juu ya taarifa za kifo chake, kwa muda mfupi niliofahamiana nae niligundua ya kwamba ni mcheshi na licha ya umri wake na nafasi yake alikuwa msikivu na anajifunza kwa kila mtu. 

Amenifanyia interview mara mbili, siku ya mwisho ilikuwa siku ya WPFD (World Press Freedom Day) Malaika Hotel, imeniuma sana, poleni waandishi wote, tuishi kwa unyenyekevu hatujui siku wala saa, mwenyezi Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi.. Aamina.
Deo Nsokolo
Rais wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania UTPC.

Salamu kutoka OJADACT
Chama cha Waandishi wa Habari wa Kupiga Vita Matumizi ya Dawa za Kulevya na Uhalifu Tanzania (OJADACT), tumeguswa kwa kiasi kukibwa na kifo cha Mwandishi wa Habari mwenzetu Charles Sokoro wa kituo cha Barmedas Jijini Mwanza. 

Tulimfahamu marehemu kwa ukarimu wake mkubwa kwa wanahabari wenzake. Alikuwa mstari wa mbele kwenye kuhamasisha jamii iache matumizi ya dawa za kulevya na uhalifu.
Alipigania uhuru wa vyombo vya Habari na haki ya kupata taarifa bila kujali vipingamizi  vilivyokuwepo.

Alikuwa mstari wa mbele kwenye kuendeleza utamaduni wa Mwafrika kwa kutoa vipaumbele kwenye ngoma za jadi.
Alikuwa fundi wa mafundi kwenye kuhamasisha Waandishi kumtumia mungu kwa kuwafundisha ujuzi wa kupiga kinanda kwenye makongamano ya kumsifu bwana.

Tunawaomba Waandishi  wote tusimame pamoja.kwenye  msiba huu wa mwenzetu, aliyefariki juzi kwenye hospitali ya rufaa ya Bugando na kesho tutamsindikiza kwenye makazi yake ya mwisho.
Tulimpenda lakini mungu alimpenda zaidi.
Edwin Soko
Mwenyekiti
OJADACT

No comments:

Powered by Blogger.