LIVE STREAM ADS

Header Ads

UTATA KIFO CHA MENEJA WA SIMBA BISCUIT JIJINI MWANZA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Utata umeibuka kufuatia kifo cha meneja wa kampuni ya utengenezaji biskuti ya Simba Biscuit mkoani Mwanza, aliekuwa amefariki nyumbani kwake mtaa wa Nyerere Road Jijini Mwanza usiku wa kuamkia jana.

Taarifa iliyotolewa jana na Kamanda wa polisi mkoani Mwanza, Ahmed Msangi, imeeleza kwamba meneja huyo, Sulesh Naranjian Somaiya (72), mwenye asili ya Asia (Hindu), majira ya saa kumi alfajiri kuamkia jana, alikutwa chooni na mdogo wake akiwa amefariki huku mwili wake ukiwa na jeraha dogo ukupande wa begani na kamba ya kiatu ikiwa shingoni.

Taarifa hiyo inaeleza kwamba, jeshi la polisi linaendelea kuwahoji ndugu wa marehemu waliokuwa wanaishi nae pamoja ambao ni mdogo wake wa kiume, shemeji yake pamoja na msaidizi wa kazi za ndani ambapo bado hakuna mtu yeyote aliekamatwa kuhusiana na tukio hilo.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya rufaa Bugando kwa ajili ya uchunguzi huku jeshi la polisi likiendelea na upelelezi kuhusiana na tukio hilo.

No comments:

Powered by Blogger.