LIVE STREAM ADS

Header Ads

VIJANA ACHENI DHANA POTOFU.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
George Binagi-GB Pazzo ambae ni Mwanahabari, Blogger na Mkulima.

Ipo dhana potofu kwa vijana wenzangu kwamba Kilimo ni Kazi ya kujitesa na haiwafai.

Niwaambie tu kwamba, kilimo kinalipa na kilimo ni sekta muhimu katika kutatua changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana nchini.
Kijana usikimbilie mjini kuuza sura ikiwa huna uhakika wa ajira za mjini. Mali iko shambani hivyo ni vyema ukajikita katika kilimo, tena kilimo cha kisasa.

Sahau kuhusu changamoto zinazotukabiri wakulima. Jitume zaidi na baada ya muda utaweza kusonga mbele kimaendeleo kupitia kilimo.

Usihofu kuhusu "bring bring" unazopenda. Mambo yamebadilika. Fanya kazi kwa ratiba. Baada ya shughuli zako za kilimo, tupia hizo "bring bring" zako.

Pamoja na kwamba mimi ni Mwandishi wa Habari/Mtangazaji na Blogger, pia mimi ni Mkulima na najivunia hilo kwani najua faida za kuwa mkulima.

Ewe kijana uliekosa ajira na umekimbilia mjini, baada ya kusoma post hii, anza kupanga ratiba za kurudi kijijini kwenu ili ukajikite katika kilimo, huko utanufaika maradufu zaidi kimaendeleo.

No comments:

Powered by Blogger.