LIVE STREAM ADS

Header Ads

WANANCHI WATAKIWA KUFUATA SHERIA ZA UHIFADHI KATIKA KUTUMIA PORI LA KIGOSI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Na Shaban Njia
Meneja wa Pori la Akiba la Moyowosi/ Kigosi lililopoa Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, Patrick Kutondolana, amewataka wananchi wanaovamia pori hilo na kufanya shughuli za kibinadamu ikiwa ni pamoja na kukata miti kwa ajili matimba katika migodi midomidogo kufuata sheria za uhifadhi.

Meneja huyo amesema kumekuwa na wimbi kubwa la kukataji wa miti katika pori hilo ambayo hutumika katika kufanyia shughuli za uchimbaji pamoja na ukaushaji wa zao la tumbaku hasa katika Wilaya ya Ushetu.

Meneja huyo aliendelea kusema kuwa baadhi ya wachungaji wa ng’ombe katika pori hilo la akiba wanatoka katika nchi za  Burundi, Rwanda, Uganda, Kenya huku watumishi wa Serikali wakijinufaisha kwa kupata kipato kupitia ng’ombe hao wanachungwa katika pori hilo.

Pia Kutondilana alisema kuwa hadi kufikia sasa tayari jumla ya ng’ombe 320 wameishataifishwa na serikali  katika wilaya ya Ushetu ambapo ng'ombe 603 nao pia wameshataifishwa na Serikali katika Wilaya ya Bukombe Mkoani Geita na kuongeza kuwa zoezi hilo litakuwa endelevu ili kuhifadhi mapori ya akiba hususani la Moyowosi/ Kigosi.

Meneja huyo alisema kuwa Pori hilo la Akiba la Moyowosi/ Kigosi  lenye ukubwa wa kilometa za Mraba 21,000 lipo katika Mikoa mitano ambayo ni Geita, Shinyanga, Tabora, Kigoma, Kagera limekuwa na changamoto nyingi inalolikumba ikiwa ni pamoja na uvamizi wa mifugo, ukataji wa miti ambayo imesababisha ukaukaji wa vyanzo vya maji.

No comments:

Powered by Blogger.