DC MTATURU ATENGA SIKU MAALUMU YA KUKAGUA SHUGHULI ZA MAENDELEO KATIKA WILAYA YAKE YA IKUNGI MKOANI SINGIDA.
Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akisisitiza jambo katika ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo Wilayani humo.
Na Mathias Canal, Singida
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akielekezwa jambo na muwekezaji wa miche ya miti Wikayani humo Mr Choi
Viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi wakikagua ujenzi wa matundu ya choo
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akipokea maelekezo ya namna ya kuitumia miche iliyooteshwa na muwekezaji Mr Choi
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu alipata nafasi ya kukutana na Club inayopambana na maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi na UKIMWI kwenye Shule ya Sekondari ya Issuna.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu Leo amekagua
miradi ya maendeleo katika kijiji cha Utaho A ambapo inajengwa shule mpya ili
kupunguza adha ya watoto kwenda umbali mrefu na kuvuka barabara ambapo pamoja
na kupatiwa mafunzo ya usalama barabarani lakini bado ni Hatari kwao.
Mtaturu amewapongeza wananchi kwa kazi nzuri wakishirikiana
na Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi Mhe Elibariki kingu na Diwani wa Kata
ya Kituntu kusimamia vyema shughuli za maendeleo na hatimaye kufanikiwa kupaua
madarasa mawili na ofisi ya walimu.
Sawia na pongezi hizo Mkuu huyo wa Wilaya amewapongeza
viongozi wote katika Wilaya hiyo kwa kusimamia ujenzi wa choo cha wanafunzi
ambacho kina jumla ya matundu 12.
Dc Mtaturu amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya
hiyo kuhakikisha serikali inaunga mkono juhudi za wananchi ili kuwasaidie
kujenga nyumba za walimu ili kufikia Januari 2017 shule ianze kupokea wanafunzi
wa darasa la kwanza.
Mkuu huyo wa Wilaya pia ametembelea vikundi viwili vilivyopo
katika Kijiji cha Makyungu, kikundi cha Muungano ambacho kinatarajia
kutotolesha vifaranga baada ya Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi kuwanunulia
mashine(Equbator )kwa thamani ya shilingi 8,700,000/- na kikundi cha pili
kinaitwa Wajefia kinachotarajia kutengeneza chakula cha kuku kwa kutumia
mashine maalumu waliyoinunua toka Shirika la Viwanda vidogo SIDO cha Mkoani
Mbeya.
Sawia na hayo Mtaturu pia amebaini Changamoto waliyonayo
ikiwa ni pamoja na elimu ya kuendesha Shuguli zao kibiashara na mtaji ambapo
amewapa nafasi ya kupeleka wajumbe watatu kwa kila kikundi kwenye viwanja vya
nane nane mjini Dodoma kwa ajili ya kupata mafunzo na mtaji wa shilingi milioni
moja kwa ajili ya kuwasaidia kuanza ununuzi wa vifaa vya kusaga chakula cha
kuku na mayai ili waanze uzalishaji wa vifaranga.
Dc Mtaturu pia amemtembelea Mr Choi raia wa Korea aliyeamua
kuanzisha kitalu cha miche ya miti na matunda kwa ajili ya utunzaji wa
mazingira katika kijiji cha Kimbwi na pia amewekeza katika elimu ambapo
anajenga shule ya Awali hadi kidato cha Sita.
Aidha Dc Mtaturu amempongeza muwekezaji huyo na kuwaalika
wawekezaji wengine kwa ajili ya kuwekeza wilayani Ikungi katika sekta
mbalimbali kwani kuna ardhi ya kutosha ambapo pia amemwagiza Mkurugenzi wa
Halmshauri kuwaelekeza watendaji wa Kata kwa ajili ya kuchukua miche ya miti na
matunda kwa Mr Choi ambaye ameamua kuungana na serikali katika kampeni ya
kutunza mazingira kwa kugawa miche bure.
"Naomba mfahamu kuwa Gharama za mashine ya kusagia chakula
cha kuku ni shilingi milioni 9.1 zilizotolewa na Halmashauri na wananchi
walichangia kujenga majengo"Alisema Mtaturu
Mtaturu pia amekagua ujenzi wa maabara uliokwama katika
Sekondari ya Mkiwa hadi umeanza kubomoka hivyo amemuagiza Diwani kukaa na Kamati
ya maendeleo ya Kata yake kuweka mikakati ya kuwashirikisha wananchi katika
Kata wapatao 2009 ili serikali iwaunge mkono kupaua na hatimaye ifikapo Januari
mwakani maabara ianze kazi.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu anatekeleza
kauli ya serikali ya awamu ya tano kwa vitendo ya Hapa Kazi Tu ambapo ametenga
Siku ya Jumapili kuwa Maalumu kwa ajili ya kukagua shughuli za maendeleo.
Katika kutembelea shughuli za maendeleo Wilayani humo pia
Mtaturu alipata nafasi ya kukutana na Club inayopambana na maambukizi ya Virusi
Vya Ukimwi na UKIMWI kwenye Shule ya Sekondari ya Issuna ambayo kitaaluma
matokeo ya kidato cha nne mwaka jana ilishika nafasi ya 10 bora.
No comments: