LIVE STREAM ADS

Header Ads

KAMPUNI YA WAJA YAENDELEA KUTOA ELIMU MBALIMBALI KWENYE MAONESHO YA NANENANE KANDA YA ZIWA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Kampuni ya Waja General inayotengeneza mabati ya Waja, Kusambaza vifaa vya maabara, vifaa vya usalama pahala pa kazi kama vile migodini, kuuza kemikali za kuchenjua dhahabu na inayomikili shule za Wasichana na Wavulana Waja, imeshiriki maonesho ya Nanenane Kanda ya Ziwa yanayofanyika kwenye Uwanja wa Nyamhongolo Jijini Mwanza.

Pichani ni Philipo Mwakabuta (kushoto) ambae ni Afisa Masoko wa kampuni hiyo Kanda ya Ziwa, akitoa maelekezo kwa wanafunzi wa shule ya wavulana Bwiru ya Jijini Mwanza juu ya shughuli zinazofanywa na Waja.
Na BMG
Banda la Kampuni ya Waja, kuna ufafanuzi wa elimu juu ya masuala mbalimbali ikiwemo elimu, afya na tahadhari pahala pa kazi
Mmoja wa wanafunzi wa shule ya wavulana ya Bwiru Sekondari akiuliza swali alipotembelea banda la Waja General Company Limited kwenye maonesho ya Nanenane Jijini Mwanza.
Wanafunzi wa shule ya wavulana ya Bwiru Sekondari wakisaini kitabu cha wageni. Kushoto ni Afisa Mauzo wa Waja General Co.Ltd, Amani Ismail.
Wanafunzi wa shule ya wavulana ya Bwiru Sekondari wakisoma vipeperushi katika banda la Waja General Company Limited.
Bonyeza HAPA Kusoma Zaidi.

No comments:

Powered by Blogger.