LIVE STREAM ADS

Header Ads

KILIMO CHA MJINI CHAWAVUTIA WATU WENGI KWENYE MAONESHO YA NANENANE JIJINI MWANZA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Tangu Agost Mosi Mwaka huu Maonesho ya Wakulima na Wafugaji yanaendelea katika Kanda mbalimbali nchini. Katika Kanda ya Ziwa Maonesho hayo yanafanyika katika Uwanja wa Nyamhongolo Jijini Mwanza ambapo yanatarajiwa kuzinduliwa rasmi kesho Agost 04,2016 na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella.
Na BMG

Katika Maonesho hayo, kuna bidhaa na mashamba darasa mbalimbali yanayooneshwa, lakini watu wengi wamevutiwa na shamba darasa la Kilimo cha Mjini kutoka kwa wajasiriamali na wakulima kutoka Buhongwa Jijini Mwanza.

Ni kilimo ambacho unaweza kukifanya ukiwa mjini kwa kutumia mifuko ama makopo ambapo unaweka udongo katika mifuko/makopo hayo na kisha kuotesha mbegu upendazo hususani za mbogamboga kama kabeji, nyanya, vitunguu, pilipili na biringanya ikiwa ni miongoni mwa mbogamboga nyingi unazoweza kuzipanda.

"Ni kilimo bora ambacho watu wengi wanaweza kukifanya kwani hakina gharama wala ugumu wowote katika kukiendesha na kinaongeza upatikanaji na ulaji wa mboga za majani ambazo ni salama". Anasema Victoria Buzare, mjasiriamali na mkulima wa Kilimo cha Mjini.

Mboga za majani zinazopandwa katika mifuko/makopo haya ni salama kwani hazitumii dawa za kemikali kuua wadudu bali katika kila kopo hupandwa mmea wa kitunguu ama tumbaku ambapo harufu ya mimea hiyo hufukuza wadudu waharibifu.
Namna shamba la Kilimo cha Mjini linavyokuwa ambapo mboga zinazopanda katika mifuko/makopo haya ni salama kwani hazitumii dawa za kemikali kuua wadudu bali katika kila kopo hupandwa mmea wa kitunguu ama tumbaku ambapo harufu ya mimea hiyo hufukuza wadudu waharibifu.
Victoria Buzare akifafanua juu ya Kilimo cha Mjini
Hellena John kutoka Buhongwa Jijini Mwanza ambae ni mshauri wa Kilimo cha Mjini anasema kilimo hiki kinafaa sana kwani ni rafiki wa mazingira na huimarisha afya za watumiaji wa mbogamboga za kilimo hiki.
Osebius Philipo ni mjasiriamali na mkulima wa Kilimo cha Mjini mbali na matumizi ya nyumbani pia kinaweza kuongeza kipato katika familia kwa kuuza mbogamboga ambazo wanafamilia wanaweza kuwa wanazilima katika muda wao wa ziada.
Kilimo cha Mjini hakihitaji eneo kubwa, maji mengi kwa ajili ya umwagiliaji wala dawa za kemikali kwa ajili ya kunyunyizia mbogamboga
Hii ni fursa mpya kwa wakazi wa mjini kujihusisha na kilimo cha aina hii kwa ajili ya kujipatia mbogamboga pamoja na kipato pia. Kumbuka kilimo hiki ni rafiki wa mazingira.
Fika katika shamba darasa la wajasiriamali na wakulima wa Kilimo cha Mjini katika Maonesho ya Nanenane Kanda ya Ziwa yanayofanyika katika Uwanja wa Nyamhongolo Jijini Mwanza.
Bonyeza HAPA Kusoma Zaidi.

No comments:

Powered by Blogger.