LIVE STREAM ADS

Header Ads

KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE KITAIFA ATAKA CHAMA CHA WATU WENYE UALBINO WILAYANI UKEREWE KUTOVURUGIKA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Kiongozi wa mbio za Mwnge Kitaifa

Na Vester Joseph - Ukerewe Mwanza
Chama cha watu wenye Ualbino wilayani Ukerewe Mkoani mwanza, kimetakiwa kujenga umoja kwa kushirikiana ili kisivurugike.

Rai hiyo ilitolewa jana na Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa 2016, George Jackson Mbijima, wakati akifungua kituo cha mafunzo ya jamii cha Umoja Training Center- UTC kilichopo wilayani humo.

Mbijima alisema kuwa mradi walio  pewa ni mradi imara wanapaswa kushirikiana na kuendeleza mradi huo pia aliwataka wananchi wakishirikiana na walemavu hao na kuacha kuwa tenge kwa ulimavu wao.

"Naombeni mpendane pia mshirikiane kulinda mradi huu najua kuna watu wataleta maneno ya kuwa chonganisha muwapuze ,ndugu zangu wananchi muwa pende hawa walemavu kwa kuwa jari na kuwapa ushirikiano wenu nao ni binadamu kama nyinyi,"Alisema Mbijima.

Awali akisoma taarifa ya Ujenzi wa kituo hicho kwa kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru kitaifa 2016 Mwenyekiti wa Chama cha Albino Wilaya ya Ukerewe Ramadhani Khalifan alisema malengo ya kituo hicho ni kuwaendeleza Albino kiuchumi na kupaza sauti dhidi ya Unyanyasaji na unyanyapaa kwa albino.

"Malengo yetu kuanzisha kituo hiki ni kutuendeleza kiuchumi sisi wa tu wenye ualbino kuelezea dunia juu ya ulinzi dhidi ya Albino na kliniki ya ugonjwa wa ngozi kwa watu wenye ualbino wapatao 87 kati yao wanaume 40 wanawake 33 na watoto 14," Alisema Khalfan.

Aidhaa tunaipongeza Serikali ya awamu ya tano ya Dk John Pombe Magufuli kwa malezi,mafunzo na usawa miongoni mwa jamii inayotuzunguka.

Ujenzi wa kituo hicho ulianza mwaka February 2014 na kukamilika june 2016 na uligharimu kiasi cha Tsh Mil 325,650,000 kati ya fedha hizo sh 650,000 ni Mchango wa Halmashauri na Tsh Mil 325,000,000 Kwa ufadhili wa Standing Voice wa Uingereza.

Kauli mbiu katika maadhimisho ya Mwenge wa Uhuru Kitaifa kwa mwaka huu ni "VIJANA NI NGUVU KAZI YA TAIFA WASHIRIKISHWE NA KUWEZESHA".
Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa, akiwa katika picha ya pamoja na viongozi pamoja na wanachama wa Chama cha watu wenye ualibino wilayani Ukerewe.
Mwenge wa Uhuru ukiwa Ukerewe mkoani Mwanza

No comments:

Powered by Blogger.